Pata taarifa kuu
VATICAN-DRC-SUDAN KUSINI

Papa Francis asikitishwa baada ya safari yake nchini DRC na Sudan Kusini kuahirishwa

Kiongozi wa Kanisa Katoliki, amesema anasikitihswa sana kwa safari yake kuzuru Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini, kuahirishwa kwa sababu za kiafya.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis AFP - VINCENZO PINTO
Matangazo ya kibiashara

Kupitia ujumbe wa video aliotua leo, Papa Francis mwenye umri wa miaka 85 amesema, anasikitika kuwa hataanza ziara hiyo katika mataifa hayo mwezi huu kama ilivyokuwa imepangwa, lakini akaongeza kuwa hivi karibuni atafanya ziara hiyo.

Papa Francis amesema anaifikiria Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa sababu ya mateso ya wananchi wake, hasa katika eneo la Mashariki mwa sababu ya utobvy wa usalama, huku akitoa wito wa amani nchini Sudan Kusini ambayo pia imeendelea kushuhudia mauaji ya raia.

Mwezi uliopita, Vatican ilitangaza kuahirisha ziara ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki, kwa sababu za kiafya kwa ushauri wa Madaktari wake ambao walisema ziara hiyo ingetatiza matibabu yake.

Mbali na Afrika, ziara yake nchini Lebanon iliahirishwa lakini mpango Wake wa kwenda nchini Canada mwishoni mwa mwezi huu, mpango umeratibiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.