Pata taarifa kuu
DRC

Watu wa kabila la Banyamulenge waishi kwa hofu mashariki mwa DRC

Nchini Jamhuri ya Congo, baadhi ya wanawake kutoka kabila la Watustsi wanaozungumza lugha ya Kinyarwanda wanaishi kwa hofu kufuatia mzozo kati ya serikali ya Kinshasa na Rwanda, kuhusu madai kuwa Kigali inawaunga mkono waasi wa M 23 Mashariki mwa nchi hiyo.

Watu wa kabila la Banyamulenge nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Watu wa kabila la Banyamulenge nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo AFP
Matangazo ya kibiashara

Chantale Murekatete ni miongoni mwa mamia ya wanawake wengine  kutoka kabila la watutsi wanaozungumza lugha ya kinyarwanda anaeleza namna anavyobaguliwa.

“Majirani wetu wanatutusi kila mara ,hata tuna woga wa kutoka nje kwa sababu wanatutizama kana kwamba hawatufahamu,” amesema .

Wiki mbili zilizopita, kumekuwa na visa vya wenyeji kuwahangaisha raia wananchi wa DRC wanaofahamika kama Banyamulenge kwa madai kuwa wanaunga mkono machafuko Mashariki mwa nchi hiyo.

Marembo Jeanine, mmoja wa msemaji wa jamii ya Watutsi anakanusha madai hayo, “Sio kweli watu wa kabila la Watusti wanaunga mkono waasi wa M 23,” amesema.

Hata hivyo, viongozi wa serikali pamoja na wale wa polisi wamesema tayari wamefanikiwa kusuka mikakati iliyo thabiti ili kuhakikisha kwamba usalama wa jamii hii unazingatiwa katika Jimbo nzima la Kivu ya Kaskazini.

 “Kwa sasa tatizo limeisha tumelitatua, amesema Job Alisa.

Haya yanajiri wakati huu ambapo maelfu ya raia waendelea kuvihama vijiji vyao wilayani utshuru kufuatia mapigano makali yanayo shuhudiwa kati ya jeshi la Congo na kundi la waasi wa M23.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.