Pata taarifa kuu
ETHIOPIA

Ethiopia yateua jopo la kufanya mazungumzo na waasi wa Tigray

Serikali ya Ethiopia imetaja ujumbe wa wasuluhishi saba, watakaoiwakilisha katika mazungumzo ya ambayo huenda yakafanyika na waasi wa Tigray.

Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Ethiopia
Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Ethiopia AFP - AMANUEL SILESHI
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huo wa serikal ya Ethiopia, utaongozwa na Naibu Waziri Mkuu Demeke Mekonnen, na hii inakuja baada ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed mapema mwezi huu kutangaza kuwa serikali yake ilikuwa imeunda Kamati ya kufanya mazungumzo na waasi wa Tigray ambao mwaka uliopita, Addis Ababa ilisema ni magaidi.

Hata hivyo, waasi hao hawajasema chochote kuhusu hatua inayochukuliwa na serikali ya Addis Ababa, isipokuwa kiongozi wa jimbo la Tigray, Debretsion Gebremichael, aliiandikia barua Jumuiya ya Kimataifa Juni 15 na kuiambia kuwa, ungozi wa Tigray ilikuwa tayari kwa mazungumzo ya wazi.

Mpaka sasa haijafahamika ni lini na wapi mazungumzo hayo yatafanyika, huku kukiwa na ripoti kuwa, wawakilishu wa Tigray wamesema wako tayari kukutana jijini Nairobi, chini ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Hatua hii inakuja, wakati msuluhishi wa Umoja wa Afrika rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, katika siku za hivi karibuni akizuru nchi hiyo kujaribu kupata mwafaka.

Mapigano kati ya wanajeshi wa serikali ya Ethiopia na waasi wa Tigray yaliyoanda Novemba 202O, yamesababsiha maelfu ya watu kupoteza maisha na mamilioni kuyakimbia makwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.