Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Polisi yaendelea kuwasaka wahalifu waliosababisha vifo vya watu 21

Polisi nchini Afrika Kusini wamekuwa wakiendelea na operesheni katika baa moja, katika mji wa Kusini wa East London, baada ya vijana 21 kupoteza maisha katika mazingira yasiyoeleweka, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Afisa wa Polisi Afrika Kusini akikagua katika eneo la usalama.
Afisa wa Polisi Afrika Kusini akikagua katika eneo la usalama. AFP - MARCO LONGARI
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema vijana 17 walipoteza maisha wakiwa ndani ya baa hiyo, huku wengine wanne wakafariki dunia wakiwa wanapata matibabu hospitalini. 

Wengine 31 wamelazwa hopsitalini wakiwa na maumivu ya mgongo, kuumwa kwa kifua, kutapika na kuumwa kichwa kwa mujibu wa maafisa wa afya, huku uchunguzi zaidi ukiendelea kubaini iwapo, pombe waliyokunywa ilikuwa na sumu. 

Vijana waliopoteza maisha hawakuwa na majeraha ypoyote na sasa maafisa wa serikali wanashuku kuwa, vifo hivyo vilisababishwa na vijana hao kunywa pombe kupita kiasi, ikizingitiwa kuwa wengu walikuwa chini ya umri wa miaka 18. 

Aidha, ripoti zinasema kuwa wengi wa vijana hao walikuwa wanafunzi waliokuwa wanasherehekea kumaliza masomo yao ya sekondari kwa kunywa pombe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.