Pata taarifa kuu

Ukraine: Zelensky kuhutubia viongozi wa Umoja wa Afrika

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajia kuhutubia viongozi wa Umoja wa Afrika Jumatatu hii, Juni 20 mchana. Kutoka mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, rais wa Ukraine atahutubia kwa njia ya video ofisi ya Baraza kuu la Umoja wa Afrika, AU, pamoja na mabalozi wa Afrika walioidhinishwa na taasisi hiyo.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mjini Kyev Ijumaa hii, Juni 17, 2022.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mjini Kyev Ijumaa hii, Juni 17, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya kwanza kwa mkuu wa nchi wa Ukraine kuzungumza na taasisi ya AU, wakati Rais wa sasa Macky Sall alitembelea Urusi hivi karibuni.

Miezi miwili na nusu iliyopita, wakati wa mazungumzo na Rais wa Senegal Macky Sall, Rais Volodymyr Zelensky alikuwa tayari ameelezea nia yake ya kuzungumza na viongozi wa Umoja wa Afrika.

Ndoto yake itatimia mapema alaasiri, Jumatatu hii. Mkutano wake wa kwa njia ya video utaonyeshwa mbele ya mabalozi wa Afrika waliokusanyika katika makao makuu ya AU mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia.

Hakuna taarifa iliyovuja juu maudhui ya hotuba yake, lakini kiongozi wa Ukraine atajaribu kuhamasisha nchi za bara hilo, hasa baada ya Aprili 7, tarehe iliyopigwa kura ya kusimamisha Urusi mbele ya Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa, ambapo nusu ya mataifa ya Afrika yalijizuia kutoa msimamo wao, anaripoti mwandishi wetu huko Addis Ababa, Noé Hochet-Bodin.

Mwanzoni mwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Umoja wa Afrika uliishtumu Ukraine kwa vya "vya kibaguzi" dhidi ya raia wa Kiafrika waliokwama nchini Ukraine.

Ukosefu wa mbolea unaweza kusababisha 'njaa ambayo inaweza kuhatarisha utulivu Afrika'

Wasiwasi mwingine wa Nchi Wanachama, usambazaji wa nafaka na mbolea za Ukraine na Kirusi, ambazo nchi nyingi za Afrika zinategemea. Macky Sall aliomba Volodymyr Zelensky siku kumi zilizopita kuondoa vizuizi kwenye bandari ya Odessa ili kuruhusu mauzo ya ngano kutoka Ukraine. Maneno ambayo tayari yamefutiliwa mbali na Kyiv, ambayo inaogopa uvamizi wa Urusi kwenye Bahari Nyeusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.