Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-WATOTO-NJAA

Maelfu ya watoto nchini Ethiopia wasumbuliwa na utapia mlo

Maelfu ya watoto nchini Ethiopia wanakabiliwa na utapia mlo, wakati huu maeneo ya Kusini na Mashariki mwa nchi hiyo yakiendelea kukabiliwa na ukame.

Watoto nchini Ethiopia wanaokabiliwa na utapiamlo kwa sababu ya baa la njaa
Watoto nchini Ethiopia wanaokabiliwa na utapiamlo kwa sababu ya baa la njaa AFP
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Save the Children, linalohusika na masuala ya watoto, linasema watoto 185,000 wanasumbuliwa na utapia mlo kwa kukosa chakula sahihi , huku wengine Elfu 50 wakihitaji kupata matibabu ya haraka. 

Jimbo la Somali ndilo lililoathiriwa zaidi na hali hii kufuatia ukame uliosababishwa na uhaba wa mvua, hali inayoelezwa kuwa mbaya ndani ya miaka 40. 

Aidha, ripoti ya Shirika hilo inaeleza kuwa kutokana na hali hiyo, watoto wanaobahatika kupata chakula, wanapata mlo mmoja tu kwa siku. 

Save the Children sasa inatoa wito kwa wahisani kujitokeza na kuokoa maisha ya maelfu ya watoto hao kwa kutoa msaada wa chakula na matibabu. 

Mbali na watoto hao, watu zaidi ya Milioni 30 wanahitaji msaada wa chakula nchini Ethiopia. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.