Pata taarifa kuu
BURKINA FASO

Polisi 11 wauawa nchini Burkina Faso na wanajihadi

Nchini Burkina Faso, wanajihadi wamewauwa maafisa 11  wa polisi Kaskazini mwa nchi hiyo karibu na nchi jirani ya Niger.

Eneo la ulinzi katika eneo la Fada N'Gourma nchini Burkina Faso
Eneo la ulinzi katika eneo la Fada N'Gourma nchini Burkina Faso AP - Sam Mednick
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa usalama wamesema, kambi ya polisi hao katika mkoa wa Seno, ilishambuliwa na wanajihadi hao usiku wa kuamkia Alhamisi na kutekeleza mauaji hayo, huku wengine wanne wakijeruhiwa.

Aidha, ripoti zinasema kuwa baada ya shambulio hilo, kuna maafisa wa usalama ambao hawajapatikana na msako wa kuwatafuta unaendelea.

Burkina Faso kwa miaka ya hivi karibuni imeendelea kukabiliwa na utovu wa usalama kwa karibu miaka saba baada ya wanajihadi kuvuka mpaka kutoka nchini Mali, na kuanza kutekeleza mauaji ya raia na maafisa wa usalama.

Kwa kipindi cha miaka saba iliyopita, watu zaidi ya 2,000 wameuwa na wengine zaidi ya Milioni 1 na Laki nane, wameyakimbia makwao kufuatia utovu wa usalama katika nchi hiyo ya Sahel.

Tangu mwezi Jánuari, nchi hiyo inaongozwa na jeshi baada ya kupinduliwa kwa rais aliyekuwa amechaguliwa na raia Roch Marc Christian Kabore kwa madai ya kushindwa kuimarisha hali ya usalama nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.