Pata taarifa kuu
VATICAN-DRC-SUDAN KUSINI

Papa Francis aahirisha ziara yake nchini DRC na Sudan Kusini

Ziara ya Papa Francis, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini, imeahirishwa kufuatia kiongozi huyo wa kiroho kusumbuliwa na goti.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis AFP - FILIPPO MONTEFORTE
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hiyo imetolewa na Vatican baada ya kile kilichoelezwa ni kutokana na ombi la Madaktari wa Papa Francis, ambao wanamfanyia matibabu ya goti.

Msemaji wa Vatican, Matteo Bruni amesema, papa Francis anasikitika kuahirisha safari hiyo iliyopaswa kufanyika kati ya tarehe 2 hadi 7 mwezi Julai, na sasa tarehe mpya itapangwa.

Papa Francis mwenye umri wa miaka 85, kwa kipindi cha wiki kadhaa sasa amekuwa akisumbuliwa na goti na mwezi uliopita alilazimika kutumia kiti cha kuwabebea wagonjwa.

Mwezi Machi, Vatican ilitangaza kuwa Papa Francis alipanga kufanya ziara barani Afrika na alikuwa ameratibiwa, kuanzia jijini Kinshasa na baadaye Goma Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na baadaye jijini Juba nchini Sudan Kusini.

Mara ya mwisho kwa DRC kutembelewa na Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani ilikuwa ni mwaka 1985 ilipotembelewa na John Paul wa pili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.