Pata taarifa kuu
DRC-MAUAJI

Watu wenye silaha wawauwa watu saba waliokimbilia usalama Mashariki mwa DRC

Watu saba waliokuwa wamekimbia makaazi yao kwa kuhofia usalama wao, wameuawa baada ya kushambuliwa na waasi wasiofahamika huko Rujagati, Wilayani Masisi, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, usiku wa kuamkia Alhamisi.

Wakimbizi wa ndani katika jimbo la Kivu Kaskazini, Mashariki mwa DRC
Wakimbizi wa ndani katika jimbo la Kivu Kaskazini, Mashariki mwa DRC UNHCR / P. Taggart
Matangazo ya kibiashara

Mauaji hayo yametokea wakati wenyeji wa kijiji cha Kashuga katika mtaa wa Mweso,  wakishangazwa na risasi kutoka kwa wahalifu hawa walioingia kwenye kamb yao ambayo inawahifadhi watu kadhaa waliokimbia makazi yao kwa sababu za ukosefu wa usalama katika vijiji vyao vya Bwito huko Rutshuru na Masisi kama alivyothibitisha Kavayama Jules kiongozi wa maeneo hayo ya Mweso.

"Watu waliuliwa wakiwa 7 waliuliwa na waasi wasiojulikana na kwasasa hali ni ya wasiwasi huko nyumbani kwetu kufwatia mauaji hayo ya raia wasiokuwa na hatua," amesema Jules.

Miongoni mwa waliouliwa ni pamoja na akina baba wanne na akina mama watatu huku wengine wakitekwa . Kahangu Tobi ni kiongozi wa shirika la raia Katika eneo hilo la Bashali Masisi.

"Eneo hili linazungukwa na Makundi mengi ya waasi lakini piya Jeshi la FARDC tunataka amani maana tunateswa," ameeleza.

Januari 25, 2021, kambi hiyohiyo ililengwa na majambazi walioua watu wawili waliokimbia makazi yao kwa mapanga baada ya kuwajeruhi wengine sita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.