Pata taarifa kuu
SOMALIA-SIASA

Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud aanza rasmi kazi

Nchini Somalia, kumekuwa na sherehe ya kumkabidhi rasmi madaraka rais Hassan Sheikh Mohamud aliyeshinda uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi uliopita.

Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud
Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud © REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Sherehe hizo zimefanyika jijini Mogadishu, na kuhudhuriwa na viongozi wa nchi jirani ambao wameahidi kushirikiana na serikali mpya ya Somalia, ili kufikia malengo ya maendeleo na usalama.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, alikuwa miongoni mwa viongozi waliohudhuria sherehe hiyo.

“Nakuhakikishia kuwa, kaka na dada zenu nchini Kenya wako tayari kushirikiana nanyi kwa ajili ya usalama na maendeleo ya ukanda wetu,” amesema Kenyatta.

Rais  Hassan Sheikh Mohamud anaingia tena madarakani, kuiongoza nchi ambayo kwa kipindi kirefu imeendelea kukabiliwa na changamoto za kiusalama kutokana na uwepo wa kundi la Al Shabab, lakini pia kwa sasa inakabiliwa na baa la njaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.