Pata taarifa kuu

Niger yasitisha mauzo ya dizeli ili kukidhi matumizi ya ndani

Uamuzi huu wa Niamey umechukuliwa kulinda matumizi yake ya ndani na kupambana na biashara ya bidhaa hiyo kwa njia isiyo halali.

Watu wakijaza mafuta kwenye pikipikizao mnamo Desemba 21, 2017 huko Niamey, Niger.
Watu wakijaza mafuta kwenye pikipikizao mnamo Desemba 21, 2017 huko Niamey, Niger. LUDOVIC MARIN/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa siku kadhaa, makundi ya wahalifu yamekuwa yakifanya biashara hiyo kuelekea nchi jirani ambazo zinakabiliwa na ugumu wa kupata biodhaa hii.

Vituo vya mafuta kwenye mipaka ya Nigeria, Benin na Burkina Faso havina mafuta. Niamey, mji mkuu wa Niger, kwa upande wake unakabiliwa na uhaba.

Kwa uzalishaji wa kila siku wa mapipa 20,000 kwa siku, Niger imekuwa nchi inayozalisha petroli kwa miaka kadhaa. Lakini kwa wiki chache zilizopita, kumekuwa na uhaba wa dizeli katika baadhi ya vituo vya mafuta ndani ya nchi, hasa katika mpaka wa Nigeria, Benin na Burkina Faso.

Katika nchi hizi tatu, lita ya dizeli inayouzwa katika kituo jirani cha mafuta ni karibu faranga 1,000 za CFA, wakati nchini Niger ni faranga 538 za CFA. Wengi pia wanakuja kutafuta bidhaa hii ya dizeli kwenye mipaka. Uhaba huo unaikabili mji mkuu, Niamey, tangu siku tatu zilizopita: hakuna tena dizeli katika vituo vingi vya mafuta, mamia ya lori kubwa zinazotumia dizeli hazitumiki.

Kwa mujibu wa Mawaziri wa Biashara na Petroli, uchunguzi wa kina umebaini kuwepo kwa uvumi kuhusu bei ya dizeli pamoja na mwanzo wa uhaba wa bidhaa hii kufuatia ulaghai wa mauzo ya kiasi kilichokusudiwa kwa matumizi ya kitaifa nje ya nchi. Kisha wizara hizo mbili ziliamua kusimamisha mauzo ya nje kuanzia Juni 1, ili kuunda hifadhi ya taifa ya usalama na kufunga vituo vya mafuta vilivyopatikana na kosa la biashara haramu ya bidhaa hiyo.

Wahusika wakuu wa uhaba huu wanatambuliwa. Ni raia wawili wa China kutoka kampuni ya kusafishia mafuta ya Zinder, Soraz, mkurugenzi wa kitengo cha mauzo na naibu wake. Wako katika mchakato wa kufukuzwa nchini Niger.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.