Pata taarifa kuu
DRC

Watu 72,000 wakimbia makwao Mashariki mwa DRC kufuatia mapigano

Mapigano kati ya wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23, ambayo yamekuwa yakiendelea wiki hii, yamesababisha watu zaidi ya Elfu 72 kuyakimbia, makwao kwa mujibu wa takwimu, zilizotolewa na Umoja wa Mataifa.

Kambi ya wakimbizi nchini DRC
Kambi ya wakimbizi nchini DRC © AFP - Alexis Huguet
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya Tume ya Umoja wa Mataifa, inayohusika na wakimbizi, imesema, maelfu ya watu hao, wameyakimbia makwao kutoka maeneo ya Rutshuru na Nyiragongo jimboni Kivu Kaskazini,  kuanzia Mei 19.

Aidha, Tume hiyo inaonya kuwa watu hao sasa wanakabiliwa mwendelezo wa ukosefu wa usalama na wizi wa mali zao, baada ya kuacha makaazi yao.

Hii inafikisha idadi ya watu waliokimbia makaazi yao Mashariki mwa DRC tangu Novemba mwaka 2021 kutokana na utovu wa usalama, kufikia zaidi ya 170,000.

Ripoti hii imekuja, baada ya Baraza la Norway linalohusika na wakimbizi kueleza pia kuwa, watu Elfu 37 wameyakimbia makwao kutoka Ruthsuru na Nyiragngo tangu Mei 22.

Leo, hali ya utulivu imeshudiwa hasa katika Wilaya za Rutshuru na Nyiragongo yaliyoshuhudia makaniliano makali wiki hii kati ya waasi wa M 23 na wanajeshi wa serikali ya DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.