Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-SIASA

Wanasiasa wanaomuunga mkono rais Touadera wapendekeza kuifanyia marekebisho Katiba

Washirika wa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadera, wamependekeza marekebisho ya katiba, yatakayomwezesja kiongozi huyo kuwania tena urais, hatua ambayo imepingwa vikali na wanasiasa wa upinzani.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati  Faustin Archange Touadéra.
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin Archange Touadéra. © Carol Valade/RFI
Matangazo ya kibiashara

Wandani wa rais Archange, wanadai hatua ya kuondoa kikomo cha mihula ya urais, hailengi kumfanya Archange mwenye miaka 65  kusalia madarakani, ila hatua hiyo inalenga kuhakikisha katiba ya Jamhuri ya Africa ya kati inafanana na ya mataifa jirani kama vile Rwanda, ambazo hazina vikomo vya muhula madarakani. 

Rais wa vyama vya upinzani humo Crepin Mboli Goumba, amesema watatumia mbinu zote kupinga mswaada huo ambao tayari umewasilishwa bungeni, amesema huenda hatua hiyo ikasabisha machafuko nchini humo. 

Mashirika ya kirai nayo yamesema hatua hiyi inarejesha nyuma demkrasia ilipingw anchini humo, yakisema mipango kama hiyo ndio imeschangia mapinduzi ya serikali katika mataiafa ya Africa magharibi kwa miaka miwili iliopita. 

Kwa mjibu wa katibu ya Jumhuri ya Africa ya kati rais anastahili kuhudumu kwa kipindi cha mihula miwili. 

Rais Archange alichaguliw mwaka 2016, baada ya mita vya wenyewe kwa wenye vilivyochangiwa na kuondolewa madarakani kwa mtangulizi wake Francois Bozize, Archange alichaguliwa tena mwaka 2020. 

Afisi ya rais nchini humo hata hivyo hajasema lolote kuhusiana na mswaada huo wa mabadiliko ya katiba. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.