Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Mafuriko mapya yasababisha uharibifu mkubwa Durban

Mafuriko mapya yametokea wikendi hii baada ya siku mbili za mvua kubwa katika  pwani ya mashariki ya nchi. Hali ni ngumu: watu mia kadhaa wamelazimika kuyahama makazi yao. Hakuna waathirika kwa sasa, lakini athari ni kubwa.

Maporomoko ya matope yalisababisha uharibifu mkubwa mnamo Mei 22, 2022 kufuatia mafuriko zaidi huko Durban, Afrika Kusini.
Maporomoko ya matope yalisababisha uharibifu mkubwa mnamo Mei 22, 2022 kufuatia mafuriko zaidi huko Durban, Afrika Kusini. AFP - RAJESH JANTILAL
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya barabara zimeharibika, madaraja yaliyoporomoka na magari yalisombwa na maji: maeneo kadhaa huko Durban yameharibiwa kabisa na mvua iliyonyesha kwa muda wa siku mbili zilizopita. Badhi ya viwanda vimeharibika. Maeneo kadhaa hayaingiliki na yanaonekana kama "visiwa", amesema waziri mkuu wa jimbo la KwaZulu-Natal.

Hakuna umeme. Wakazi kadhaa wamekwama na wameshindwa kuondoka makwao."Maji na matope yamepanda hadi ghorofa ya 2 ya jengo langu... Hatuwezi kutoka,"  Kevin Govender ameliambia shirika la habari la AFP. Ilitubidi tusubiri msaada ufike.

Takriban watu 250 walihamishwa usiku kucha kutoka Jumamosi hadi Jumapili.

Shughuli za uokoaji ziliendelea wikendi nzima. Vituo 82 vya mapokezi vilifunguliwa kwa haraka ili kuwahudumia waathiriwa.

Mwishoni mwa mwezi Aprili, mvua kubwa ilisababisha karibu waathiriwa 450. Wakati huo Rais Cyril Ramaphosa alitangaza hali ya janga la asili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.