Pata taarifa kuu

Uhusiano kati ya Rwanda-Burundi kuimarika zaidi: Rais Ndayishimiye.

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, ametangaza kuwa uhusiano kati ya Rwanda na Burundi utakuwa mzuri zaidi iwapo watu waliopanga na kufadhili mapinduzi ya kijeshi ya 2015 wanaodhaniwa kuwa wako mafichoni jijini Kigali watarejeshwa jijini Gitega kufunguliwa mashtaka.

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye
Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye AFP Photos/Tchandrou Nitanga
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika Ikulu yake jijini Bujumbura,Jumanne ya wiki hii rais Ndayishimiye alieleza kuwa Burundi inafanya mazungumzo na mamlaka nchini Rwanda ilikuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ya Afrika mashariki ambao umeyumba kwa kipinidi cha miaka 7 iliyopita.

Mataifa hayo jirani hayajakuwa na uhusiano mzuri kwa miaka kadhaa sasa, Burundi ikifunga mipaka yake na Rwanda ikipiga marafuku uuzaji wa matunda na mboga jijini Kigali tangu mwaka wa 2016.

Tangu kuingia madarakani kwa rais Ndayishimiye 2020, uhusiano kati ya Kigali na Bujumbura umeonekana kuanza kuimarika kwa kiasi kikubwa.

Ujumbe wa watu wa ngazi ya juu wa mataifa hayo mawili wakiwemo wakuu wa intelejensia na magavana wamekuwa wakikutana kwa lengo la kujenga urafiki tena.

Waziri mkuu wa Rwanda Edouard Ngirente, alifanya zaira jijini Bujumbura wakati wa sherehe za siku ya uhuru wa Bujumbura Julai 2021. Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa afisa wa ngazi ya juu wa Rwanda kuzuru Burundi tangu mzozo kwa kisiasa kuanza kati yao mwaka wa 2015.

Mwaka wa 2021, Burundi katika taarifa yake ilisema kuwa juhudi kubwa zilikuwa zimepigwa kuelekea uimarishwaji wa amani na usalama kati ya Rwanda na Burundi.

Burundi ilitoa mchango mkubwa kwa Rwanda wakati ambapo iliwakamata na kuwakabidhi kwa Kigali magaidi waliokuwa wanapanga shambulio nchini Rwanda.

Rwanda na yenyewe Julai 2021 iliwakabidhi Burundi watu 19 wenye silaha waliokuwa wametekeleza shambulio nchini Burundi na baadae kutorekea nchini Rwanda .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.