Pata taarifa kuu

Kenya: William Ruto anatarajiwa kumtaja mgombea mwenza wake .

Naibu rais wa Jamuhuri ya kenya William Ruto ambaye anawania urais katika uchaguzi wa agosti 9 mwaka huu, anatarajiwa kumeteua mgombea mwenza Jumamosi Mei 14.

Kenyan Deputy President William Ruto
Kenyan Deputy President William Ruto file.jpg
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa tume huru ya uchaguzi na mipaka katika taifa hilo la Afrika mashariki, wagombea urais wanapaswa kuwa wametangaza majina ya wagombea wenza wao kabla ya Jumatatu Mei 16.

Mgombea wa urais kupitia tiketi ya Azimio la Umoja-One Kenya ,Raila Odinga naye anatarajiwa kumtaja mgombea mwenza wake Jumapili Mei 15 shughuli inayotarajiwa kufanyika katika uwanja wa kihistoria wa Kamkunji.

Ruto anakutana na viongozi wa mrengo wake wa Kenya kwanza katika makaazi yake rasimi katika eneo la Karen kabla ya kumtangaza mgombea mwenza wake. Ruto anatarajiwa kumtaja kati ya Seneta Kithure Kindiki na mbunge Ndindi Nyoro kuwa mgombea wake wa urais.

Jopokazi la kuwapiga msasa watu wanaotaka kuwa wagombea wenza wa Odinga katika uchaguzi wa agosti tayari likiwa limependekeza majina ya kiongozi wa chama cha  Narc Kenya  Martha Karua, Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka pamoja na mbunge wa zamani wa eneo bunge la  Gatanga  Peter Kenneth kwa Odinga ambaye atamchagua mtu anayemtaka.

Joto la kisiasa linaendelea kupanda kuelekea uchaguzi wa mwezi agosti, ushindani mkubwa ukiwa kati ya naibu wa sasa wa rais William Ruto na kinara wa chama cha ODM waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.

Martha karua , waziri wa zamani wa mswala ya katiba na haki akipigiwa upatu kuwa mgombea mwenza wa Odinga. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.