Pata taarifa kuu

Mali: Mnadhimu mkuu wa jeshi amehitimisha ziara nchini Rwanda

Mnadhimu mkuu wa jeshi la Mali, Jenerali Oumar Diarra, alhamis Mei 12 amehitimisha ziara ya siku tatu ya kikazi nchini Rwanda, ambapo pia alikutana na rais Paul Kagame, lengo likiwa ni kuimarisha uhusiano wa kiusalama baina ya nchi zao.

Wanajeshi wa Mali wakipiga doria.
Wanajeshi wa Mali wakipiga doria. © AFP/Souleymane Ag Anara
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa ziara yake, Jenerali Oumar Diarra alikutana na rais wa Rwanda Paul Kagame, pamoja na mkuu wa mkuu wa majeshi ya Rwanda, Jean Bosco Kazura, ziara ambayo ililenga kuimarisha ushirikiano wa  kiusalama na ulinzi kati ya nchi hizo.

Katika mahojiano na runinga ya kitaifa ya Rwanda, Jenerali Diarra alizungumzia juu ya utulivu wa Rwanda na makadirio ya jeshi lake, na hasa nchini Msumbiji, kabla ya kuorodhesha malengo ya jeshi la Mali.

Kulingana na watafiti, kuwasili kwa ujumbe wa Mali nchini Rwanda juma hili ni ishara kuwa utawala wa Bamako umetambua kutengwa kwake, na hivyo Bamako inajaribu kutafuta uhusiano wa kidiplomasia na baadhi ya nchi za Afrika.

Akizungumza na wanahabari, Diarra ameeleza kuwa Mali inatarajia kujifunza mambo muhimu kutokana na uimara wa Rwanda ambapo wanatarajia kufanya ushirikiano wa wa maswala mbalimbali ikiwemo mafunzo ya kijeshi.

Kiongozi huyu amesema kuwa katika siku zijazo wanatarajia kutia saini mikataba ya ushirikiano wa kijeshi ya kati ya nchi hizo mbili,ushirikiano wa kijeshi ambao amekiri kuwa ni muhimu kwa mataifa ya bara Afrika katika vita dhidi ya makundi ya kijihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.