Pata taarifa kuu

Sudan Kusini: Zaidi ya visa 700-vya dhuluma za kimapenzi chini ya miezi 3: UN

Ripoti ya Ujumbe wa umoja wa mataifa nchini Sudan Kuisni (UNMISS), inasema kuwa zaidi ya raia 700 wamedhulumiwa kimapenzi katika robo ya kwanza ya mwaka huu wakati huu pia nchi hiyo inaposhuhudia machafuko ya kikabila.

Askari wa umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, wakipiga doria kwenye kambi yao, Julai 20, 2016.
Askari wa umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, wakipiga doria kwenye kambi yao, Julai 20, 2016. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Aidha ripoti hiyo ya UN inaeleza kuwa licha visa vya mashambulio yanayotekelezwa kwa raia kuripotiwa kupungua nchini Sudan kusini, ripoti za dhuluma za kijinsia zimeongezeka mara mbili zaidi ya ilivyoripotiwa mwaka jana.

Tangu Januari hadi Machi, UNMISS, imedhibitisha visa 63 vya dhuluma za kimapenzi ilinganishwa na ilivyoshuhudiwa mwaka wa 2021 ambapo visa 28 vilisajiliwa.

Makundi ya waasi na maofisa wa kiusalama wakiripotiwa kuwa katika mstari wa mbele katika utelezaji wa dhuluma za kimapenzi kwa asilimia 64.

Maeneo ya Jonglei Equatoria mashariki na majimbo ya Warrap, maeneo ambayo yanashuhudia mapigano ya kikabila yakitajwa kuongoza kwa visa vya dhuluma za kimapenzi.

Waangalizi wa UN wameeleza kuwa mabadiliko ya tabia nchi na ukosefu wa maeneo ya malisho ni baadhi ya mambo yanayochangia katika machafuko ya kikabila nchini Sudan Kusini.

Mkuu wa UNMISS nchini Sudan Kusini Nicholas Haysom ameeleza kuwa UN itaendelea kuangazia pakubwa visa vya dhulma za kimapenzi kwenye taifa hilo.

Kituo kinachoshugulikia wahanga wa dhulma za kimapenzi katika hosiptali ya rufa ya Equatoria ya kati jijini Juba kimesajili visa 29 vya dhulma za kimapenzi ikiwemo kisa cha mtoto miaka miwili aliyedhulumiwa Januari mwaka huu.

Idadi kubwa ya visa hivi vya dhuluma za kimapenzi vikiripotiwa jijini Juba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.