Pata taarifa kuu

Ziara ya Samia: Tanzania yabadili msimamo wake kuhusu sukari ya Uganda.

Nchi ya Tanzania itaanza tena kununua sukari kutoka nchini Uganda baada ya marufuku ya karibu miaka mitatu, hatua inayokuja baada ya ziara ya rais Samia Suluhu Hassan nchini Uganda ambapo amekutana na rais Yoweri Museveni.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Β© blog.ikulu.go.tz
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inayoashiria kulegezwa kwa moja ya migogoro ya kibiashara kati ya nchi hizo Afrika mashariki, iliodumu kwa karibu miaka mitatu, ambapo viongozi wa nchi hizo wamekubaliana kuondoa vikwazo visivyo na kodi kati yao ili kuinua biashara.

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliotolewa baada ya viongozi hao kukutana hapo siku ya jumanne ya tarehe 10 mwezi huu, Uganda itasambaza tani elfu 10 za sukari ili kuziba pengo la uzalishaji wa bidhaa hiyo nchini Tanzania.

Wakati wa ziara yake ya kitaifa ya siku mbili nchini Uganda, rais Samia, alikubaliana na mwenyeji wake, rais Yoweri Museveni kuwa Kampala pia itaisambazia Tanzania dawa za kupunguza makali ya HIV.

Kwa miaka sasa, Uganda imekuwa ikiilaumu Tanzania kwa kuweka vikwazo visivyo na kodi kwenye bidhaa za sukari na maziwa ambavyo vimezuia biashara kati ya nchi hizo mbili.

Tangu kuingia madarakani rais Samia , amekuwa mbioni kurejesha uhusiano ulionekana kuyumba kati ya Tanzania na majirani zake wakati wa utawala wa hayati John Pombe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.