Pata taarifa kuu

Tatizo la usalama mashariki wa DRC. Kwa nini mauaji yanaedelea?

Kumekuwa na hali ya sintofahamu kuhusu mauaji yanayoshuhudiwa mashariki mwa DRC ambapo mamia ya watu wameendelea kupoteza maisha na wengine wakilazimika kuyatoroka makwa ili kuokoa maisha yao. Muandishi wetu 

Kundi la waasi wa APCLS katika eneo la Masisi mashariki mwa DRC.
Kundi la waasi wa APCLS katika eneo la Masisi mashariki mwa DRC. © ©Facebook
Matangazo ya kibiashara

Wakati mauaji hayo yakiendelea Wahusika wakuu wamekuwa wakitajwa kuwa ni watu kutoka makundi mbalimbali, wakiwemo waasi wa ADF pamoja na CODECO, na kundi la M23 waliotajwa hivi karibuni.

Makundi hayo kwa asilimia kubwa yanaundwa na raia wa Congo na wanaofariki ni wacongo kiasi cha kuzua maswali kwanini wanatekeleza mauaji dhidi ya ndugu zao?

Nani yuko nyuma ya makundi hayo ambayo yameendelea kusababisha madhila miongoni mwa wananchi mashariki wa DRC?

Mauaji ya mwishoni mwa juma kuamkia juma hili yamezua maswali chungu nzima yaliokosa majibu. Zaidi ya watu 100 wameuawa huko Ituri wakiwemo watoto, kundi la waasi wa CODECO wakitajwa kuhusika. Kwanini mauaji hayo?

Watu hawa wanaopoteza maisha wamekosea nini?

Zaidi ya kinachozungumzwa kuhusu mauaji hayo ni kwamba waasi wa CODECO ambao wanaelezwa kuwa kabila la walendu walikabiliana na waasi kiutoka kabila la wahema kuwania kisima cha uchimbaji madini, lakini hadi kushambulia kambi ya waliohama makwao?

Vikosi vya usalama ambavyo jukumu lao ni kuwalinda raia na mali zao, wanafanya nini kuzuia mauaji?

Serikali ya Congo kwa nini haionekani kuguswa zaidi na kuchukuwa hatuwa madhubuti juu ya kinachoendelea mashariki mwa Congo?  

Mauaji hayo yanaendelea kuripotiwa huku kukiwa na kikosi kikubwa zaidi duniani cha kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa ambacho lengo kuu na kulinda na kuzuia mauaji dhidi ya wananchi wa Congo.

kwa vyovyote vile, ipo siku ukweli utafahamika kuhusu mauaji hayo licha ya kuchelewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.