Pata taarifa kuu

Tanzania na Uganda zatiliana saini mikataba kadhaa ya ushirikiano.

Uganda na Tanzania, zimetiliana saini mikataba kadhaa ya ushirikiano, ikiwa ni pamoja na Tanzania sasa kuendelea kununua sukari  na dawa za kupunguza makalu ya maambukizi ya virusi vya ukimwi ARV’s kutoka nchini Uganda. 

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni. via REUTERS - PRESIDENTIAL PRESS SERVICE
Matangazo ya kibiashara

Hii imekuja, kufuatia ziara ya siku mbili ya rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan hapa Uganda ambapo Imekubaliwa kuwa  Uganda itaiuzia Tanzania tani Elfu 10 ya sukari, hatua ambayo imemfurahisha rais Museveni na kuisifia nchi hiyo jirani.  

 Tangu tuingie Serikalini, tumekuwa tukifanya kazi vizuri sana na Serikali za Tanzania na  viongozi waliokuwepo. Hatuna tatizo  na Tanzania kwa sababu hakuna mvutano kati ya Tanzania na Uganda. Kwa hiyo kazi yetu ni kuzingatia zaidi usalama, miundombinu na biashara 
00:18

Yoweri Museveni kuhusu biashara na Tanzania Mei 11 2022

Kauli hii imeungwa mkono na rais Samia, ambaye nchi yake imeingia kwenye mkataba na Uganda yakujenga bomba la mafuta kutoka Hoima mpaka bandari ya Tanga, ambao viongozi wanasema mchakato unaendelea vema licha ya kupingwa na waharakati wa mazingira na wale wa haki za binadamu. 

 Nchi zetu mbili zimeamua kulipea swala la  Biashara na Uwekezaji kipau mbele. Hatua mahususi zitachukuliwa ili kurahisisha biashara kati ya nchi zetu hasa uondoaji wa vikwazo visivyo vya ushuru. Nawaalika Waganda kuja Tanzania kwa ajili ya kuongeza biashara na uwekezaji.
00:21

Samia Suluhu Hassan akiwa ziarani nchini Uganda Mei 11 2022

 Yasin Nasser ni mfanyabiashara kutoka kampuni ya mafuta, anataka vikwazo zaidia vya kufanya biashara viondolewe.   

 

Nadhani wanashugulikia vizuri bomba la mafuta  itakua inaongeza biashara lakini muhimu tunataka wa punguze garama za barabarani.
00:08

Yasin Nasser mfanyabiashara

Takwimu zinaonesha kuwa kwa kipindi cha  miaka 25 iliyopita, mauzo ya Uganda kwenda  Tanzania yameongezeka kutoka Dola Milioni 2 nukta 6 hadi Dola Milioni 95.1. Nayo Tanzania, iliuza bidhaa vyenye thamani ya Dola Milioni 734 mwaka 2020.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.