Pata taarifa kuu

Uganda yawachia huru wanafunzi wavuvi raia wa kenya kutoka gereza la Luzira

Wanafunzi wa nne raia wa kenya kutoka katika kaunti ya Busia eneo jirani na taifa la Uganda, ambayo  kwa muda wamekuwa wakizuiliwa katika gereza la Luzira nchini humo baada  kukamatwa kwa kosa ya kuingia katika maji ya Uganda wakati walipokuwa wakivua samaki kwenye ziwa Victoria  hatimaye wameaachia huru baada ya kulipa faini.

Wavuvi katika ziwa victoria.
Wavuvi katika ziwa victoria. sarahemcc/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Wanafunzi hao wameondoka nchini Uganda baada ya kulipa faini ya shillingi elfu 50 pesa za kenya ($431) kila moja baada ya kuwa kizuizini kwa mwezi moja baada ya kukamatwa walipokuwa wanavua samaki katika ufuo wa Bumbe kaunti ndogo ya Funyula kaunti ya Busia nchini kenya.

Miongoni mwa walioaachiwa huru ni pamoja na Stephen Barasa mwanafunzi wa shule ya upili ya  Sisenye , Joseph Sande, mwanafunzi wa darasa la nane katika shule ya msingi ya Busembe , Derick Ouma na Polycarp Makokha wote waliokamilisha mtihani wao wa kidato cha nne mwaka jana katika shule ya upili ya  Busijo. 

Wanafunzi hao wameeleza changamoto walizokumbana nazo wakati wakiwa gerezani nchini Uganda, swala la msongamano wa wafungwa katika gereza la Luzira likitajwa kuwa miongoni mwa matatizo waliokumbana nayo.

Mwanafunzi wengine wawili, Bernard Ouma na Meshack Odero, waliokamatwa pamoja na wavuvi wengine 12 wanagali wanazuiliwa nchini Uganda, taarifa zikieleza kuwa wavuvi wengine 92 raia wa kenya wanagali wanazuiliwa katika gereza la Luzira.

Rfi Kiswahili awali ilizuru ziwa Victoria katika eneo la Busia ambapo ilikutana na wavuvi kutoka katika baadhi ya fuo ikiwemo Omena beach, Mulukhoba beach ambapo wavuvi wa Kenya walielezea changamoto wanazopitia mikononi mwa wanajeshi wa Uganda wakati wakiwa katika shughuli zao za uvuvi.

Swala la kutokuwepo kwa ishara za kuwaelekeza wavuvi iwapo wanakaribia katika maji ya Uganda lilitajwa kuwa tatizo pamoja na ukosefu wa vifaa vya kisasa vya kuvua samaki, viongozi wa fuo hizi kwa mara kadhaa wamekuwa wakifanya mikutano ya kuhusisha wavuvi ( BMU) wa pande zote kenya na Uganda ilikuwapa mafunzo kama njia moja ya kuepukana na changamoto wanazokabiliana nazo wakiwa kazini.

Uganda kwa muda sasa imekuwa ikiwatuhumu wavuvi kutoka kenya kwa kuingia katika maji yake bila ya ruhusu ambapo pia wanalaumiwa kwa kutumia baadhi ya vifaa vilivyo chini ya kiwango kuvua, bidhaa ambazo zinadaiwa kuwanasa samaki wadogo  na kuchafua mazingira swala ambalo ni kinyume na sheria za uvuvi.

Idadi kubwa ya raia katika kaunti ya Busia, wanategemea pakubwa uvuvi wa samaki  kutoka ziwa victoria kama kitega uchumi ila kutokana na idadi ndogo ya maji yanayomilkiwa na kenya, baadhi yao hujikuta wakiwa katika maji ya nchini jirani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.