Pata taarifa kuu

Rais Samia yuko nchini Uganda kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Rais wa jamuhuri ya Tanzania, Samia Suluhu, ameanza ziara ya  kikazi Jumanne mei 10 nchini Uganda  kwa siku mbili kufuatia mwalikio mwa mwenyeji wake rais Yoweri Museveni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. © https://www.ikulu.go.tz/
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na mkurugenzi wa mawasiliano katika ofisi ya rais nchini Tanzania Zuhura Yunus, ziara hii inalenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili za Afrika Mashariki.

Rais Samia na mwenyeji wake rais Yoweri Museveni wanatarajiwa pia kujadiliana kuhusu maswala ya kawi, biashara, usafiri, afya pamoja na ushirikiano kati ya mambo mengine muhimu.

Hii ni ziara ya pili kwa rais Samia nchini Uganda tangu kutangazwa  rais wa taifa hilo mwezi machi mwaka wa 2021 kufuatia kifo cha rais John Magufuli.

Ziara yake nchini Uganda, inakuja baada yake kutangaza ahueni kwa raia wa taifa hilo siku ya jumatatu swala alilosema ni njia ya kuwakinga watanzania kutokana na makali yanayotokana na ongezeko la bei ya mafuta, ahueni inayoaanza kutumika rasimi Juni 1.

Tangazo hili la rais Samia likija kutokana na ongezeko la bei ya mafuta nchini Tanzania na baadhi ya mataifa ya Afrika mashariki yakiwemo kenya, Rais Samia akisema swala hili limeathiri mataifa maskini na tajiri kote duniani.

Serikali za Uganda, Tanzania na kampuni ya mafuta ya Ufaransa ya TotalEnergies mwezi feburuari zilitiliana saini makubaliano ya ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi.

Wachambuzi wa mambo wanahisi kuwa huenda rais Samia anarejea nchini Uganda kukagua mradi huo wa ujenzi wa bomba hilo la kusafirisha mafuta, rais Samia akiwa tayari amezuru mataifa mengine barani Afrika yakiwemo Kenya ambapo alikutana na rais Kenyatta.

Ziara hii inakuja wakati huu Kenya nayo ikiwa imechukua hatua ya kumaliza mzozo wa kidplomasia kati yake na Uganda kutokana na hatua ya kenya kutangaza kuuza nchini humo mafuta yaliokuwa yanapaswa kusafirishwa kwenda jijini Kampala.

Kenya, mwezi jana iliwaagiza wasambazaji kuuza lita milioni 133.5 za mafuta aina ya supa petrol na lita milioni 104.7 za mafuta aina ya disel nchini humo, mafuta yaliokuwa yamepangiwa kwenda nchini Uganda, swala lilozua ghadhabu kutoka kwa wabunge jijini kampla kutokana na upungufu wa bidhaa hiyo.

Uganda inategemea kenya kwa usafirishaji wa asilimia 72 ya bidhaa za mafuta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.