Pata taarifa kuu

Rais wa Somalia Mohamed Farmajo kuwania kwa muhula wa pili katika uchaguzi ujao.

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi, anayejulikana pia kama Farmajo, ametangaza kuwania tena kwa muhula wa pili.

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, maarufu kama  Farmajo
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed, maarufu kama Farmajo Riccardo Savi / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Alhamisi iliyopita, kamati ya bunge inayohusika na kuandaa uchaguzi huo ilitangaza kuwa uchaguzi wa urais kwenye taifa hilo la pembe ya Afrika utafanyika tarehe 15 Mei.

Muhula wa Rais Farmajo ulimalizika Februari mwaka jana lakini alibakia mamlakani wakati huu pia kukishuhudiwa hali ya kucheleweshwa kwa uchaguzi wa wabunge nchini humo.

Rais Farmajo anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa wagombea kadhaa wakiwemo marais wawili wa zamani.

Nchini Somalia, rais huchaguliwa na wabunge na masenet na Ili kuchaguliwa, mgombea lazima apokee angalau theluthi mbili ya kura, au kura 184.

Mataifa ya magharibi yakiongozwa na Marekani, yamekuwa yakisisitiza mara kwa mara mamlaka nchini Somalia kukamilisha mchakato wa uchaguzi, wakisema kuwa ucheleweshaji wa kufanyika kwa uchaguzi unarudhisha nyuma vita muhimu dhidi ya uasi kutoka kwa wapiganji  wa al-Shabaab.

Somalia kwa miaka sasa imekuwa ikipitia wakati mgumu wa hali ya kutokuwa na utulivu na inakabiliwa na uasi wa Waislam wenye itikadi kali Shebab, wanaohusishwa na kundi la  al-Qaeda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.