Pata taarifa kuu

Afisa wa zamani wa Rwanda amefikishwa mahakamani mjini Paris Ufaransa.

Afisa mwandamizi wa zamani wa Rwanda Laurent Bucyibaruta amefikishwa mahakamani mjini Paris, akituhumiwa kuhusika na mauaji ya halaiki ya watu kwenye taifa hilo la Afrika, Kiongozi huyo wa ngazi ya juu nchini humo alikuwa bado hajakabiliwa na haki nchini Ufaransa kutokana na mauaji ya mwaka 1994.

Picha yenye majina ya watu walioaangamia katika mauwaji ya kimbari nchini Rwanda.
Picha yenye majina ya watu walioaangamia katika mauwaji ya kimbari nchini Rwanda. AFP/Jacques NKinzingabo
Matangazo ya kibiashara

Kesi hiyo ya Laurent Bucyibaruta, iliyofunguliwa Jumatatu, inatarajiwa kudumu kwa miezi miwili na kushirikisha mashahidi zaidi ya 100, wakiwemo walionusurika kutoka Rwanda ambao wamesafiri kwa ndege au watahudhuria kwa njia ya video.

Kesi ya Bucyibaruta ni ya nne kutoka kwa mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa mahakamani nchini Ufaransa, ambayo kwa muda mrefu imekuwa chini ya shinikizo kutoka kwa wanaharakati kuchukua hatua dhidi ya washukiwa wa uhalifu ambao walikuwa wamekimbilia katika ardhi ya Ufaransa.

Takriban Watutsi 800,000 na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliangamia katika siku 100 za mauaji mwaka 1994 ambapo wanamgambo wa Kihutu waliwaua Watutsi waliokuwa wakijificha makanisani na shuleni.

Bucyibaruta mwenye umri wa miaka 78 anakabiliwa na kifungo cha maisha jela iwapo atapatikana na hatia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.