Pata taarifa kuu
BURKINA FASO

Watu 11 wauawa baada ya kushambuliwa na wanajihadi nchini Burkina Faso.

Jeshi nchini Burkina Faso, limedhibitisha kuuwawa kwa wanajeshi wake saba wakiwemo wengine wanne wa dharura katika mashambulio mawili tofauti kaskazini mwa taifa hilo.

Vita dhidi ya makundi ya kijihadi nchini Burkina Faso.
Vita dhidi ya makundi ya kijihadi nchini Burkina Faso. AFP
Matangazo ya kibiashara

Shambulio la kwanza lilitokea siku ya Alhamis karibu la mji wa Solle, ambapo wanajeshi wawili waliuwawa pamoja na raia wengine watano wanaosaidia wanajeshi wa serikali katika vita dhidi ya wanajihadi, wanajeshi wengine watano wakiuwawa siku hiyo hiyo katika eneo la Ouanobe kwa mujibu wa tarifa ya jeshi.

Makundi ya kijihadi yanayohusishwa na kundi la kigaidi la Al-Qaeda na lile la Islamic State, kwa muda sasa yamekuwa yakitekeleza mashambulio katika maeneo ya kaskazini na mashariki mwa Burkina Faso tangu mwaka  2015.

Zaidi ya watu 2,000 wakiuwawa katika mashambulio yanaotekelezwa na wanajihadi hao ambapo watu wengine zaidi ya milioni mbili wakiripotiwa kuyama makwao, wengi walioathiriki wakiwa ni wanawake na watoto.

Mataifa kadhaa ya Afrika yakiwemo Mali, Nigeria yamekuwa yakitatizwa na makundi ya wanajihadi kwa muda sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.