Pata taarifa kuu
SOMALIA-SIASA

Uchaguzi wa urais nchini Somalia kufanyika Mei, 15

Kamati ya bunge la Somalia inayoshughulikia masuala ya uchaguzi imetangaza kwamba uchaguzi wa urais nchini humo hatimaye utafanyika Mei 15 mwaka huu baada ya kuchelewesha kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Wabunge nchini Somalia
Wabunge nchini Somalia AP - Farah Abdi Warsameh
Matangazo ya kibiashara

Kupitia taarifa kwa televisheni ya taifa, kamati hiyo  imesema wabunge na maseneta watamchagua rais Jumapili ijayo mei 15.

Uchaguzi nchini Somalia, imechelewesha kutokana na vita vya  kisiasa mara kwa mara na rais Mohemed Abdullah Farmajo, anayetafuta muhula wa pili madarakani, na Waziri Mkuu Hussein Roble kukosa kuelewana.

Washirika wa kimataifa wa Somalia, wamekuwa wakishinikiza kufanyika kwa uchaguzi huo, hofu ikiibuka kuwa huenda kucheleweshwa kwa uchaguzi huo zaidi kukainyima Somalia, ufadhili wa Dolla millioni 400, kutoka kwa shirika la fedha duniani, hatua mambayo itatumikiza Somalia kwenye mgogoro zaidi.

Tangazo la kufanyika kwa uchaguzi wa Urais nchini Somalia ni afueni kwa raia wa taifa hilo na washirika wake wa kimataifa, wakati huu Somalia ikikabiliwa na utovu wa Usalama na baa la njaa, watoto wakiwa kwenye hatari zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.