Pata taarifa kuu
SUDAN-USALAMA

HRW lataka viongozi wa mapinduzi Sudan kuacha kuwafanyia vitisho waandamanaji

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linaitaka Jumuiya ya Kimataifa, kuwashinikiza viongozi wa kijeshi nchini Sudan kuacha kuwakamata na kukiuka haki za wanaharakati wanaopinga mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea mwaka uliopita.

Waandamanaji wanaounga mkono demokrasia waandamana katika mitaa ya Khartoum Jumatatu Oktoba 25, 2021 kupinga mapinduzi ya kijeshi.
Waandamanaji wanaounga mkono demokrasia waandamana katika mitaa ya Khartoum Jumatatu Oktoba 25, 2021 kupinga mapinduzi ya kijeshi. AP - Ashraf Idris
Matangazo ya kibiashara

Wakati hayo yakijiri, ripoti zinasema mapigano zaidi ya kikabila yameripotiwa Magharibi mwa jimbo la Darfur na kwa kipIndi cha wiki moja, iliyopita, watu 200 wameuawa. 

Emily Wambungu kutoka Shirika la Madaktari wasiokuwa na mipaka MSF, anasema mbali na muaji kuna majeruhi wengi. 

Wagonjwa ni wengi sana. Sehemu ya wagonjwa waliojeruhiwa wakingoja matubabu imejaa. Kuna wagonjwa mia-mbili ambao wanangoja kuhudumiwa. 

Msemaji wa serikali ya jimbo la Darfur   Abubaker Bakri, anasema wanatiwa wasiwasi na kuendelea kwa mauaji hayo. 

Tumeingiwa na wasiwa mkubwa kuhusu  kile kitaletwa na mapigano haya, hasa kwa watu waliolazwa kwenye zahanati, watu ambao kamwe hawawezi kupata matibabu wanayohitaji kutokana na uharibufu wa hospitali. 

Mauji haya yamesbababisha maelfu ya watu kuyakimbia makwao. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.