Pata taarifa kuu

Malaria yaendelea kusababisha vifo vingi duniani

Dunia inapoadhimisha siku ya kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Malaria, Shirika la afya duniani linasema watu zaidi ya 627,000 walifariki dunia mwaka 2020, wengi wakiwa ni kutoka Afrika.

Mhudumu wa afya akijiandaa kutoa dozi ya chanjo dhidi ya malaria huko Ndhiwa, Kenya.
Mhudumu wa afya akijiandaa kutoa dozi ya chanjo dhidi ya malaria huko Ndhiwa, Kenya. AFP - BRIAN ONGORO
Matangazo ya kibiashara

Malaria bado inaorodhesha kwenye nafasi ya pili ya magonjwa yanayosababisha vifo vingi baada ya magonjwa yanayoathiri mfumo wa kupumua. 

Tarehe 25 Aprili ni siku ya Malaria duniani wakati ambapo Shirika la Afya duniani (WHO) hutoa uelewa kwa jumla kuhusu juhudi za pamoja na kuiepusha dunia na malaria.

Zaidi ya kuongezeka kwa viwango vya joto dunaini, watafiti wanaonya kwamba kupungua kwa viwango vya mvua na unyevu nyevu na hata hali ya ukame pia kunaweza kusababisha ukuaji wa wa haraka wa mbu wanaobeba ugonjwa katika maeneo ambayo haukuwahi kuripotiwa kabla.

WHO imetangaza hivi karibuni kuwa zaidi ya watoto milioni moja katika mataifa ya Ghana, Kenya na Malawi wamekwishapokea dozi moja au mbili za chanjo ya kwanza ya dunia ya malaria, chini ya mpango ulioratibiwa na shirika hilo la Umoja wa Mataifa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.