Pata taarifa kuu

DRC: Kanisa Katoliki latoa wito kwa mapadre ambao ni baba wa familia kuacha kazi zao za kidini

Suala la useja wa mapadre wa Kikatoliki limekuwa ni gumzo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Waraka wa Baraza la Maaskofu CENCO umevuja katika vyombo vya habari. Waraka huo ambao umetiwa saini na maaskofu wote wa nchi hiyo, unawataka mapadre wa Kongo ambao wana mtoto mmoja au wengi kuachana na kazi zao za kidini.

CENCO inadai usafi wa kikuhani kutoka kwa mapadre wake.
CENCO inadai usafi wa kikuhani kutoka kwa mapadre wake. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

CENCO inadai usafi wa kikuhani kutoka kwa mapadre wake. Katika hati ya kurasa 19 yenye kichwa “Katika shule ya Yesu Kristo. Kwa maisha ya kweli ya ukuhani”, maaskofu wa Kongo wanazungumza juu ya "kutoingiliana" kwa majukumu ya kiongozi familia na ukuhani. Kwa hivyo, inaombwa kwa kila padre au kiongozi yoyote wa kidini katika kanisa katoliki nchini DRC "kustaafu kwa kazi ya kidini na kusimamia majukumu yake kama baba wa familia".

CENCO inakwenda mbali zaidi. Ikiwa kiongozi huyo wa kidini atakataa kuachia ngazi, askofu ataweza kuwasilisha faili kwa Vaticani na kuomba adhabu ya juu zaidi, sawa na kufukuzwa moja kwa moja katika shuguli za Kanisa.

Jambo hilo si geni, hata kama viongozi wa Kikatoliki wa nchini DRC wanabaki kimya mara nyingi juu ya aina hii ya mambo. Wengine wanashangaa ikiwa maagizo haya mapya ya CENCO yalikuwa hayajaanza kutumika. Kwa hakika, katika siku za hivi majuzi, visa kadhaa vya mapadre waliofukuzwa kazi zao vimefichuka. Siku chache zilizopita, viongozi watatu wa Dayosisi ya Tshumbe, katikati mwa nchi, walitengwa na uamuzi wa Vatican. Uamuzi thabiti kwani mmoja wa mapadre watatu alitangaze kwamba hakuwahi kuhukumiwa au kusikilizwa.

Sehemu ya waraka wa CENCO pia inawahusu watoto wa mapadre hao wa Kikatoliki pamoja na mama zao. Baraza la Maaskofu linasema linataka "kuvunja ukimya" kuhusiana na hali yao, likikumbusha kwamba kwa ujumla "walinyanyapaliwa na jamii". "Tuna wajibu wa kimaadili kutambua kuwa watu hawa wapo na wanateseka kimyakimya," imesema CENCO.

"Tunaona kwamba kuna nia hii ya kuunganisha watoto waliozaliwa kati ya mapadre na wanawake, wanaonyanyapaliwa. Katika jamii ya Kongo, wanachukuliwa kuwa watoto waliozaliwa kwa njia ya dhambi..." ,  amesema Lucie Sarr, mratibu wa La Croix Africa, tovuti ya habari ya kidini ya gazeti la La Croix lenye makao yake barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.