Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Mali: Human Rights Watch yalaani mauaji ya zaidi ya watu 300 huko Moura

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSMA, bado inasubiri idhini kutoka kwa mamlaka ya mpito kuzindua kazi yake ya kutafuta ukweli huko Moura, kijiji kinachopatikana katikati mwa Mali, ambacho kilikabiliwa na operesheni kubwa ya kijeshi Machi 23 na Machi 31.

Gari la jeshi la Mali huko Timbuktu, Septemba 9, 2021.
Gari la jeshi la Mali huko Timbuktu, Septemba 9, 2021. AFP - MAIMOUNA MORO
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Mali limebaini kwamba liliwaua wanajihadi 203 na limewakamata takriban hamsini, lakini vyanzo vingi vya ndani na vya kibinadamu, vya Mali na kimataifa, vinashutumu mauaji ya halaiki ya raia. Jumanne hii, Aprili 5, 2022, shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch limeshutumu "mauaji" katika ripoti ya kutisha.

"Niliishi kwa hofu kila dakika, kila sekunde, nikifikiria zamu yangu nitakamatwa na kuuawa. Ushahidi huu ni mmoja wa jumbe zilizokusanywa na shirika la Human Rights Watch kutoka kwa watu 27 - wakazi wa Moura, wafanyabiashara waliokuwepo sokoni, wawakilishi wa jamii pamoja na vyanzo vya kidiplomasia na usalama. Kulingana na ushuhuda huu, sio watu 203, lakini angalau watu 300 - vyanzo vingi hata huenda mbali ya takwimu hii - ambao waliuawa huko Moura na askari wa Mali na wasaidizi wao wa kutoka Urusi.

Mashahidi wanathibitisha kwamba miongoni mwa wale waliouawa, baadhi yao walikuwa wanajihadi, walionyooshewa kidole na wakazi, lakini kwamba kwa wengi wao walikuwa raia: "waliuawa kwa sababu walikuwa na ndevu nyingi na suruali fupi", ameelezea mtu aliyenusurika, ambaye amebainisha kuwa wakazi walilazimika kufanya hivyo.

Kwa miaka kadhaa, Moura imeishi chini ya vitisho vya magaidi ya kundi la Katiba Macina, lenye mafungamano na kundi la GSIM ambalo mara kwa mara huja kijijini kuchukua zaka, kuhubiri na kuchukuwa chakula.

HRW yaataka uchunguzi ufanyike

Manusura wengine wanaonyesha wazi kulengwa kwa kabila la Fulani na wanajeshi wa Mali na wanamgambo wa Urusi. Ushahidi sawia ulikuwa umekusanywa wakati wa shutuma za awali za unyanyasaji katika maeneo mengine katikati mwa Mali katika miezi ya hivi karibuni, hasa katika eneo la Ségou.

Warusi walikuwa wengi zaidi kuliko wanajeshi wa Mali huko Moura. Angalau katika siku za kwanza za operesheni. Ushuhuda uliokusanywa na shirika la Human Rights Watch unataja wanamgambo mia moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.