Pata taarifa kuu

Mkurugenzi wa UNICEF aanza ziara ya siku nne nchini DRC

Mmarekani Catherine Russel, Mkurugenzi Mkuu wa Unicef, alianza ziara yake ya kwanza nchini DRC siku ya Jumapili na kwa siku nne katika nchi ambayo watoto ni waathiriwa wa ghasia za makundi yenye silaha. UNICEF ​​​​ilifanya siri ziara hii iliyoanzia katika mji wa Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini ambao uko chini ya sheria za jeshi kwa miezi 11.

Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF Catherine Russel alizuru Kabul nchini Afghanistan Februari 25, 2022.
Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF Catherine Russel alizuru Kabul nchini Afghanistan Februari 25, 2022. AP - Hussein Malla
Matangazo ya kibiashara

Kwanza atakutana kwa mazungumzo na Bintou Keita, mwakilishi wa Monusco, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo ambao ulisema Jumapili kwamba unataka kukabiliana na mzizi na sababu za kimuundo za ukosefu wa usalama. Catherine Russel atapokelewa na gavana wa mkoa wa Kivu Kaskazini ambapo kuni la M23 limeanzisha tena yanayotia wasiwasi mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Kati ya mikoa ya Ituri na Kivu Kaskazini zaidi ya watoto 17,000 wameachiliwa kutoka kwa makundi yenye silaha tangu mwaka 2017, lakini ni watoto wangapi ambao bado wanaajiriwa kwa nguvu?

Mkurugenzi wa Unicef ​​​​atataka kujua kinachoendelea kuhusiana na miradi inayofadhiliwa na shirika hilo, hususan ule wa kupeleka maji ya kunywa katika viunga vya Goma au hospitali ya Heal Africa ambayo imekuwa ikiwatibu wanawake waathiriwa kwa miaka mingi.

Aidha, Umoja wa Mataifa hivi karibuni umepaza sauti kutokana na kuzuka kwa ghasia zinazofanywa na wanamgambo wanaowaua raia waoishi katika kambi za waliokimbia makazi yao.

Mkurugenzi mkuu mpya wa UNICEF ​​​​atamaliza ziara yake ya siku nne katika mji mkuu wa Kinshasa ambapo atakutana na Rais Félix Tshisekedi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.