Pata taarifa kuu

Ajali ya helikopta ya Monusco huko DRC: FARDC na M23 washutumiana

Walinda amani nane walifariki dunia Jumanne Machi  29 katika ajali ya helikopta ya Monusco, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC. Helikopta hiyo ilianguka mashariki mwa nchi hiyo, katika eneo ambalo mapigano makali yamekuwa yakiendelea kwa siku kadhaa kati ya wanajeshi wa DRC na waasi wa M23. Pande zote mbili zinashutumiana kila mmoja kwa kuiangusha helikopta hiyo.

Helikopta ya MONUSCO.
Helikopta ya MONUSCO. Photo MONUSCO/Force
Matangazo ya kibiashara

Pamoja na vita vya ardhini, kumeibuka vita vya maneno. Kwa upande wa wanajeshi wa DRC wanasema, waasi wa M23 ndio waliangusha helikopta hiyo, wakati kulingana na Kinshasa, chombo hiki kilikuwa kikifanya kazi ya upelelezi isiyo na madhara ili kutathmini hali ya ukimbizi iliyosababishwa na mapigano.

Waasi wamekanusha tuhuma hizo, wakisema kuwa hayo ni "madai ya uongo" ili kuzua. Kwa mujibu wa M23, askari wa DRC ndio walioiagusha helikopta hiyo. Wakati FARDC ikirusha makombora dhidi ya kijiji cha Tchanzu, helikopta ya Monusco ilipigwa kombora kutokakambi ya kijeshi ya Rumangabo, kulingana na kundi la M23.

Wanajeshi sita wa Jeshi la Anga la Pakistani na waangalizi wawili wa kijeshi, Mrusi na Mserbia, walifariki dunia katika ajali hiyo. Miili yao ilirejeshwa Goma, ikisubiri kusafirishwa katika nchi zao. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa umefungua uchunguzi wa pamoja na Kongo tangu tukio hilo lilipotokea.

Kwa sasa, Monusco inabaki kuwa angalifu. Inasema tu kuwa chanzo cha tukio hilo hakijulikani kwa sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.