Pata taarifa kuu

Ukraine yaamua kuondoa kikosi chake Walinda amani DRC

Wanajeshi mia mbili na hamsini wa Ukraine kwa sasa wako mjini Goma na wanashiriki katika kikosi cha Umoja wa Mataifa, MONUSCO. Kwa sababu ya vita katika nchi yao, Kiev imeamua kuwarudisha nyumbani wanajeshi wake. Umoja wa Mataifa unajaribu kutafuta suluhu ili kuchukua nafasi ya kikosi hiki, ambacho kilikuwa kinatoa usaidizi muhimu wa vifaa.

Ukraine ilikuwa na wanajeshi 250 kwa vikosi vya MONUSCO.
Ukraine ilikuwa na wanajeshi 250 kwa vikosi vya MONUSCO. MONUSCO/Force MONUSCO
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa na wanajeshi 250 kati ya kikosi cha wanajeshhi 14,000, Ukraine iko mbali na nchi kumi zinazoongoza kwa kuchangia wanajeshi. Hata hivyo, kikosi hiki kinajumuisha sehemu muhimu ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa, kwa sababu Kiev hutoa helikopta nane kati ya 24. "Ni muhimu hasa kwa usafiri wa vifaa, katika eneo ambalo miundombinu ni dhaifu sana", duru za kuaminika zinabaini.

Wanajeshi wa Ukraine ni muhimu sana kwa kusafirisha dawa au kusafirisha wanajeshi na maaafisa wa polisi wa DRC wanaotumwa katika maeneo ya kivita. Pia wana jukumu muhimu katika kuanzisha SDC, vituo vidogo vilivyowekwa karibu na maenro ya kivita kwa wiki kadhaa wakati ghasia zinapozuka.

Hata hivyo, askari wa Ukraine wanaondoka, lakini pia helikopta zao, vifaa vyao na wafanyakazi wanaohusika na huduma mbalimbali wanaondoka. "Si jambo la kushangaza na ni haki yao kuondoka, hata kama haifanyi kazi kuwa rahisi," amesema afisa mmoja wa Monusco.

Mada hiyo kwa sasa inajadiliwa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York na uwakilishi wa Ukraine. Lengo ni kufafanua ratiba ya kuondoka, kutatua masuala ya kisheria na kupunguza athari kwenye ujumbe huo. Mataifa mengine Wanachama kwa vyovyote vile yatawasiliana ili kuchukua nafasi ya Ukraine na kuepusha ombwe lenye matatizo kwa walinda amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.