Pata taarifa kuu

Baraza jipya la mawaziri latangazwa huko mashariki mwa Libya

Baraza jipya la mawaziri  nchini Libya limeidhinishwa na Bunge la Libya lenye makao yake makuu mashariki mwa nchi hiyo,hatua ambayo inaweza kuzua wakati wowote mvutano mkubwa na serikali ya umoja wa kitaifa inayoongozwa na Abdulhamid Dbeibah huko Tripoli.

Walibya waandamana kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi wa Urais uliokuwa umepangwa kufanyika Desemba 24, huko Benghazi, Libya, Desemba 24, 2021.
Walibya waandamana kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi wa Urais uliokuwa umepangwa kufanyika Desemba 24, huko Benghazi, Libya, Desemba 24, 2021. REUTERS - ESAM OMRAN AL-FETORI
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na spika wa bunge Aguila Saleh, wajumbe 92 ndio wameidhinisha Jumanne wiki hii baraza hilo jipya litakaloongozwa na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Fathi Bashagha.

Kubuniwa kwa serikali ya Bashagha kunaashiria mawaziri wakuu wawili nchini humo suala ambalo wachambuzi wanasema huenda likazua upya ghasia nchini humo.

Mwanzoni mwa mwezi Februari, Bashagha alipewa jukumu la kuunda serikali mpya itakayochukua nafasi ya ile ya Dbeibah ambayo ilibidi kuondoka madarakani baada ya uchaguzi uloahirishwa mwezi wa Desemba. Dbeibah amerudia mara kadhaa kusema kwamba ataacha madaraka baada ya uchaguzi mkuu na kukabidhi utawala kwa seriali iliochaguliwa na raia.

Dbeibah ambaye pia ni tajiri mkubwa wa ujenzi alichaguliwa mwaka mmoja uliyopita ikiwa sehemu ya juhudi za Umoja wa Mataifa za kurejesha utulivu nchini humo kufuatia mapinduzi ya mwaka wa 2011, yaliomuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu Moamer Kadhafi.

Jukumu kubwa la Dbeibah lilikuwa ni kuongoza taifa hilo kwenye uchaguzi mwezi Decemba, lakini ukaahirishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.