Pata taarifa kuu

Côte d’Ivoire: Raia watiwa wasiwasi kuhusu kupanda kwa bei za bidhaa

Nchini Côte d'Ivoire, kupanda kwa bei za bidhaa za kimsingi kumesababisha raia kutoa maoni mbalimbali. Mafuta ya kupikia, nyama, mchele, petroli, au vitoweo vimepanda bei  hivi majuzi kuanzia %10 hadi 40, huku mwaka wa 2021 tayari ukiwa na ongezeko la jumla la bei.

Mwanamume anauza mkate katika soko la Abobo huko Abidjan.
Mwanamume anauza mkate katika soko la Abobo huko Abidjan. AFP PHOTO/ ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Shirikisho la wanunuzi nchini Côte d'Ivoire sasa linaiomba serikali kuchukua hatua kutokana na kuzorota kwa ununuzi.

Suala hili limekuwa ni gumzo nchini Côte d'Ivoire. Ongezeko la hivi majuzi la bei ya mafuta, kutoka faranga za CFA 615 hadi faranga 635, na bidhaa za kimsingi, hususan nyama ya ng'ombe na mafuta ya kupikia, vinauzwa kwa bei ghali . Jean-Philippe Koffi, kiongozi wa muungano wa mashirika ya wanunuzi nchini Côte d'Ivoire, sasa anaiomba serikali kuchukua hatua. Kulingana na yeye, kuzuiwa kwa muda wa bei ya baadhi ya bidhaa za watumiaji haitoshi tena.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.