Pata taarifa kuu
LIBYA-SIASA

Waziri Mkuu mpya achaguliwa na wabunge nchini Libya

Wabunge nchini Libya, wamemteua aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani Fathi Bashagha kuwa Waziri Mkuu mpya, uamuzi ambao unatarajiwa kuzua mvutano zaidi wa kisiasa katika taifa hilo la Afrika Magahribi.

Fathi Bashagha, aliyechaguliwa na wabunge kuwa Waziri Mkuu
Fathi Bashagha, aliyechaguliwa na wabunge kuwa Waziri Mkuu Abdullah DOMA AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Bashagha alipitishwa kwa kauli moja na wabuge hao, uamuzi ambao hata hivyo unatarajiwa kuzua mvutano wa uongozi kati yake na Waziri Mkuu Abdulhamid Dbeibah, anayeongoza serikali ya pamoja jijini Tripoli inayoungwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa.

Waziri Mkuu huyo anayeongoza serikali jijini Tripoli, kabla ya uamuzi wa wabunge ambao hufanya vikao vyake katika mji wa Tobruk,  Mashariki mwa nchi hiyo, aliapa kutokabidhi madaraka kwa yeyote ambaye hajachaguliwa kupitia kwa wananchi.

Baada ya kushindwa kuandaa uchaguzi mwezi Desemba mwaka uliopita, wabunge wakiongozwa na Spika Aguila Saleh, waliapa kuiondoa serikali hiyo ya pamoja.

Umoja wa Mataifa na Mataifa ya Magharibi, yamemtaka Dbeibah, ambaye msafara wake ulishambuliwa mapema siku ya Alhamisi kuendelea kuwa madarakani mpaka Uchaguzi utakapofanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.