Pata taarifa kuu
MALI-MAZUNGUMZO

Mali: Serikali na makundi yenye silaha wafikia makubaliano

Makubaliano yalitiwa saini Jumatano jioni kati ya serikali ya mpito ya Mali na makundi yenye silaha yaliyotia saini makubaliano ya amani.

Kanali Ismael Wague, anazungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya CNSP huko Kati, Septemba 16, 2020.
Kanali Ismael Wague, anazungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya CNSP huko Kati, Septemba 16, 2020. AFP - MICHELE CATTANI
Matangazo ya kibiashara

Makundi yenye silaha yaliyokusanyika ndani ya muungano wa CSP na Waziri ya Maridhiano ya Kitaifa, Kanali Ismaël Wagué, walitia saini hati hiyo Jumatano jioni baada ya siku kadhaa za mashaka juu ya ushiriki wa Waziri katika majadiliano haya yaliyofanyika huko Roma, kwa mwaliko wa shirika moja nchini Italia.

Hati hiyo inayoitwa "Mkataba wa msingi wa Roma" inalenga kumaliza mzozo ambao ulianza mwezi Oktoba. Waziri wa Maridhiano ya Kitaifa wa Mali kisha alikosoa hatua zilizochukuliwa na muungano wa waasi wa CSP, ambao unaleta pamoja makundi yenye silaha kutoka Kaskazini yaliyotia saini makubaliano ya amani ya mwaka 2015: waasi wa zamani kutoka kundi la CMA na makundi mengine ambayo yamekuwa yakitetea umoja wa Mali.

Mamlaka ya mpito ilichukua mtazamo hafifu wa Mfumo huu ulioundwa miezi michache mapema huko Roma, chini ya mwamvuli wa shirika la Ara Pacis, linalojulikana kuwa karibu na serikali ya Italia na idara ya ujasusi na ambalo pia linapambana dhidi ya uhamiaji haramu.

Miezi minne iliyopita, Kanali Wagué aliomba kwamba mungano wa waasi wa CSP ukomeshe ziara zake kwa viongozi wa nchi jirani. Kwa hasira, makundi yenye silaha yalimtaka kwa kauli moja ajiuzulu.

Jamaa wa waziri pia anaeleza kwamba Kanali Ismaël Wagué alisita kwa muda mrefu kabla ya kwenda Roma, CSP ikichukuliwa kuwa tishio kwa umoja wa nchi ya Mali. Makundi yenye silaha yaliyotia saini, ambayo yaliwasili Roma wikendi hii na kumngoja waziri huyo kwa siku tatu, yanathibitisha kwamba CSP inalenga kuwezesha utekelezwaji wa makubaliano ya amani ya mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.