Pata taarifa kuu

Berlin yatiwa mashaka juu ya kujitolea kwake katika ukanda wa Sahel

Ujerumani inasema ina wasiwasi kuhusu hali nchini Mali na inatafakari kuhusu mustakabali wa kujitolea kwake katika ukanda wa Sahel, ikiwa ni muhimu zaidi kwa Jeshi la Ujerumani - Bundeswehr - nje ya nchi.

Mwanajeshi wa Ujerumani akitafuta sehemu kulikotegwa bomu lililotengenezwa kienyeji wakati wa doria kwenye barabara ya Gao - Gossi mnamo 2018.
Mwanajeshi wa Ujerumani akitafuta sehemu kulikotegwa bomu lililotengenezwa kienyeji wakati wa doria kwenye barabara ya Gao - Gossi mnamo 2018. AFP Photo/Seyllou
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano, Februari 2, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani alionyesha mashaka yake kuhusu uendelevu wa ahadi ya Berlin kwa Mali. Waziri atakuwepo leo nchini Mali.

"Kwa kuzingatia mipango ya hivi karibuni ya serikali ya Mali, lazima tujiulize ikiwa juhudi zetu za pamoja zinaweza kuambatana na mafanikio": Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock alielezea mashaka yake siku ya Jumatano kuhusu kujitolea kwa nchi yake nchini Mali.

Wiki mbili zilizopita, Waziri wa Ulinzi alikataa kujiondoa kwa Ujerumani nchini Mlai. Lakini hali inabadilika na wengi wanazidi kuwa na mashaka. Hususan wabunge wanaosimamia suala hili. Kwa sababu nchini Ujerumani, Bundestag, Baraza la Wawakili,  linaidhinisha na kuongeza upya mamlaka ya Jeshi la Ujerumani - Bundeswehr - nje ya nchi.

Kura inahitajika tena mwezi wa Mei. Jeshi la Ujerumani- Bundeswehr - limekuwepo huko kwa takriban miaka tisa na kwa sasa karibu wanajeshi 1,200 katika kikosi cha Minusma na zaidi ya 300 kwa ujumbe wa mafunzo ya Umoja wa Ulaya kwa jeshi la Mali. Shughuli za Bundeswehr kwa sasa zimepunguzwa kutokana na vikwazo vilivyowekewa Bamako.

Waziri Katja Keul anayehusishwa na Mambo ya Nje anaenda nchini Mali leo. Atakutana na serikali ya Mali, lakini pia wawakilishi wa mashirika ya kiraia. Berlin haitafanya uamuzi peke yake na inasisitiza juu ya haja ya kuratibu na washirika wake, ikianza na Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.