Pata taarifa kuu
LIBYA-UCHAGUZI

Libya yahitaji Waziri Mkuu mpya baada ya kumalizika kwa muhula wa Abdelhamid Dbeibah

Bunge la Libya, lililokutana Jumatatu, Januari 31, huko Tobruk, mashariki mwa nchi hiyo, lilitangaza ufunguzi kwa wagombea kwenye nafasi ya Waziri Mkuu, kuchukua nafasi ya Abdelhamid Dbeibah kama waziri mkuu wa serikali ya mpito.

Waziri Mkuu wa Libya Abdel Hamid Dbeibah wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Tripoli,  Februari 25, 2021.
Waziri Mkuu wa Libya Abdel Hamid Dbeibah wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Tripoli, Februari 25, 2021. AP - Hazem Ahmed
Matangazo ya kibiashara

Madaraka ya Dbeibah kinadharia yalimalizika Desemba 25 na Bunge lilikuwa tayari limetaja masharti ya kuwania kwenye wadhifa wa Waziri Mkuu. Zaidi ya yote ni suala la kutia saini ahadi ya kutogombea uchaguzi ujao wa urais. Hatua hii inawagawanya wabunge na huenda ikazidisha vita vya kuwania madaraka.

Wagombea watakaokuwa wametimiza vigezo watahojiwa mnamo Februari 7. Waziri Mkuu mpya atateuliwa haraka.

Kwa mujibu wa taarifa zetu wagombea wanane tayari wamewasilisha maombi yao kwa spika wa Bunge. Miongoni mwao ni maafisa kutoka magharibi mwa Libya, ikiwa ni pamoja na waziri wa zamani wa mambo ya ndani, Fathi Bachagha.

Bunge la Libya, likijikita katika maandishi ya makubaliano ya kisiasa yaliyotiwa saini huko Geneva mwishoni mwa mwaka 2020, linabaini kwamba mamlaka ya waziri mkuu wa sasa yalimalizika kufuatia kuahirishwa kwa uchaguzi.

Abdelhamid Dbeibah anakosolewa kwa kutaka kusalia madarakani kwa muda mrefu iwezekanavyo. amekuwa akitangaza kwamba atakabidhi madaraka kwa serikali tu itakayochaguliwa. Jumatatu, Januari 31, akijibu tangazo la Bunge, alijibu kwamba “serikali itaendelea kutekeleza majukumu yake hadi uchaguzi utakapofanyika”. Alikariri kuwa jumuiya ya kimataifa inasitasita na mabadiliko hayo.

Msemaji wa bunge alibaini kwa upande wake kwamba "baadhi ya mabalozi" pamoja na mshauri wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Libya wametakiwa "kutoingilia masuala ya Libya".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.