Pata taarifa kuu

Mapinduzi Burkina Faso: Mkanganyiko juu ya hatima ya Rais aliyeondolewa madarakani

Tangu mapinduzi ya kijeshi nchini Burkina Faso, Rais aliyeondolewa madarakani Roch Marc Christian Kaboré hajajitokeza tena na hajazungumza hadharani. Hali bado tete, hata kama vyanzo kadhaa vinaonyesha kuwa anazuiliwa na jeshi, lakini yuko katika afya njema.

Rais wa Burkinabe Roch Marc Christian Kaboré, Novemba 28, 2017.
Rais wa Burkinabe Roch Marc Christian Kaboré, Novemba 28, 2017. LUDOVIC MARIN / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kelele nyingi, uvumi mwingi ulienea kama kawaida katika masaa yaliyotangulia na kufuatia mapinduzi ya kijeshi, hata hivyo hakuna uhakika kuhusu hatima ya Roch Marc Christian Kaboré. Inajulikana tu kwamba askari waliozungumza kwenye televisheni ya taifa, Jumatatu jioni, Januari 24, walitangaza kwamba wameamua kusitisha madaraka ya rais wa Jamhuri.

Kulingana na mmoja wasaidizi wake, Roch Marc Christian Kaboré yuko chini ya ulinzi wa jeshi katika sehemu isiyojulikana, lakini anazuiliwa katika mazingira mazuri, katika jumba la kifahari. Hana nia ya kuondoka nchini. Asubuhi, chanzo cha kidiplomasia kilithibitisha kwamba rais Kaboé hajafanyiwa dhulma yoyote wala kunyanyaswa wala kutishiwa usalama wake.

Barua ya kujiuzulu haijathibitishwa

Viongozi wa mapinduzi wa MPSR walithibitisha jana kwamba mapinduzi yao yalifanyika "bila kumwaga damu na bila vurugu zozote na unyanyasaji kwa wale waliokamatwa, wanaozuiliwa mahali salama". Lakini mashaka yaliendelea baada ya milio ya risasi kusikika karibu na makazi ya rais usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu na picha za viti vya gari vikiwa na damu ambazo zilikuwa zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Kutokuwa na uhakika bado kunaendelea kuhusu kujiuzulu kwa Roch Marc Christian Kaboré. Barua iliyoandikwa kwa mkono ambayo ina saini yake na ambayo iliwekwa kwenye ukurasa wa Facebook wa shirika la utangazaji la RTB bado haijathibitishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.