Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron: "Kipaumbele chetu ni kumpa hadhi yake Rais Kaboré kama rais

Rais wa Ufaransa amejibu, Jumanne hii, Januari 25, 2022, kuhusiana na hali nchini Burkina Faso, katika mahojiano na RFI, siku moja baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini humo ambapo wanajeshi walitangaza kuwa wamemuondoa madarakani rais Roch Marc Christian Kaboré.

Rais wa Burkina Faso Roch March Christian Kaboré na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwenye mlango waIkulu ya Élysée, Desemba 17, 2018.
Rais wa Burkina Faso Roch March Christian Kaboré na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwenye mlango waIkulu ya Élysée, Desemba 17, 2018. ludovic MARIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Akihojiwa kuhusu msimamo wa Ufaransa baada ya matukio ya Jumatatu hii nchini Burkina Faso, Rais Emmanuel Macron amesema: "Ufaransa, kama unavyojua, iko katika eneo hilo kupambana dhidi ya ugaidi. Na mara kwa mara, nimejitolea kuwa pamoja na mamlaka za kikanda.

ECOWAS ililaani mapinduzi haya mapya jana Jumatatu, kwa hakika, yakiongozwa na jeshi. Na Rais Kaboré akiwa amechaguliwa kidemokrasia na raia wake mara mbili, Ufaransa inaunga mkono msimamo wa ECOWAS. Kipaumbele chetu ni wazi kwamba kwanza kabisa, apewe hadhi yake kama rais wa jamhuri na kurejesha hali kuwa tulivu. Ni mapema sana leo kuingia kwa undani zaidi, ikiwa naweza kusema hivyo, katika uainishaji wa hali nchini Burkina Faso. Na ni wazi kuwa hali hii bado inatia wasiwasi kutokana na kile kilichotokea tangu majira ya joto ya mwaka 2020 nchini Mali, kile kilichotokea katika miezi ya hivi karibuni nchini Guinea. Na nadhani kwamba eneo hilo lazima liungwe mkono katika nia yake ya kudumisha mabadiliko ya kiraia na uchaguzi wa kidemokrasia. Sambamba na hayo, ningependa kukumbusha hapa kwamba kipaumbele chetu katika eneo hili ni dhahiri kuendelea kupambana na ugaidi wa Kiislamu, ambao unaendelea kuleta uharibifu nchini Mali, lakini pia nchiniBurkina Faso, ambayo imekuwa ikilengwa na mashambulizi mengi ya kigaidi hivi karibuni. Zaidi ya hayo, tunapoyatazama madai, sababu ambazo zimetolewa na jeshi ni wazi kwamba hali ya usalama jaribio hili la mapinduzi ya jeshi na maandamano ya raia dhidi ya makundi hayo ya kigaidi ni sababu ya uasi huu. Kwa hivyo dhamira yetu iko katika uhusiano wa karibu na ECOWAS kwa upande mmoja, lakini washikadau wote, kundi linaloitwa Initiative Accra, linalopambana dhidi ya aina zote za ugaidi katika ukanda huo, na kuwa upande wa serikali na raia.

Kuondolewa madarakani kwa Rais Roch Kaboré ni mapinduzi ya nne Afrika Magharibi ndani ya miezi 17 iliyopita.

Nchi jirani ya Mali imeshuhudia mapinduzi ya kijeshi mara mbili katika kipindi hicho, yakichochewa na wasiwasi juu ya kutoweza kukabiliana na kuongezeka kwa ghasia za wanamgambo wa Kiislamu.

Kutokana na mapinduzi hayo, mipaka ya ardhi na anga imefungwa kuanzia usiku wa manane, serikali na Bunge vimevunjwa na katiba kusitishwa. Amri ya kutotoka nje imewekwa kuanzia saa tatu usiku hadi kumi na moja alfajiri.

Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari imetiwa saini na kiongozi wa MPSR Luteni-Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba ambaye anaibuka kama shujaa mpya wa nchi hiyo.

MPSR imesema itapendekeza kwa muda mwafaka, ratiba ya kurejea kwa utaratibu wa kikatiba unaokubaliwa na wote. Lakini pia wametetea hatua yao ya mapinduzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.