Pata taarifa kuu
DRC-HAKI

DRC: Mahakama yafungua kesi dhidi ya Sud-Oil na Egal baada ya uchunguzi wa Congo Hold-up

Mahakama mjini Kinshasa, nchini DRC, imeanzisha kesi dhidi ya kampuni ya mafuta ya Sud-Oil na Egal, kampuni mbili zinazodaiwa kumilikiwa na rais wa zamani Joseph Kabila na jamaa zake. Baada ya kelele na kufichuliwa, sasa ni mwanzo wa mchakato ambao unaweza kusababisha utaratibu wa kisheria.

Kinshasa, mji mkuu wa DRC.
Kinshasa, mji mkuu wa DRC. Wikimedia/CC
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kampuni ya mafuta ya Sud-Oil na kampuni ya kuagiza nyama na samaki ya Egal kutajwa katika uchunguzi mkuu wa Kongo Hold-up,  mahakama ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congoimeamua kujihusisha na kesi hiyo. Faili imefunguliwa hivi punde kuhusu kampuni hizi mbili. Ni kwa mlahakama kuthibitisha madai yaliyomo katika uchunguzi uliochapishwa na vyombo vya habari kadhaa vya kimataifa, ikiwa ni pamoja na RFI, anaelezea mtaalamu wa sheria.

Na iwapo uhalifu unaotangazwa utathibitishwa, mahakama italazimika kwenda hatua nyingine, yaani kufungua daftari la mwendesha mashtaka wa umma, amesema mtaalamu huyo wa sheria . Mtaalam huyo wa sheria anaongeza kuwa itakuwa muhimu kutarajia mashtaka iwezekanavyo na uwezekano wa kukamatwa kwa watuhumiwa, kabla ya kutuma faili mbele ya mahakama yenye uwezo.

Mamilioni ya dola za pesa za umma zilifujwa

Kulingana na waandishi wa uchunguzi wa Congo Hold-up, hati zilizopatikana zinaonyesha ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma. Wanatajwa, miongoni mwa wanaodhaniwa kunufaika, rais wa zamani wa Jamhuri, Joseph Kabila na jamaa zake. Sud-Oil na kampuni zake za tanzu, kulingana na uchunguzi, zimepokea zaidi ya dola milioni 90 za pesa za umma. Wakati, kulingana na waandishi wa uchunguzi huo, dola milioni 43 kutoka Benki Kuu zilikwenda, kwa ushirikiano na benki ya BGFI, kwa kampuni ya kuagiza nyama na samaki ya Egal.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.