Pata taarifa kuu

Uhaba wa mafuta DRC: Serikali kutangaza bei mpya katika kipindi cha saa 48

Serikali itatangaza ndani ya saa 48 muundo mpya wa bei ili kukabiliana na uhaba wa mafuta na kupunguza kupanda kwa bei ya mafuta kwenye vituo vya ununuzi wa mafuta katika maeneo ya kusini na mashariki mwa DRC. Hayo yametangazwa na Waziri wa Uchumi Jean-Marie Kalumba Yuma, mwishoni mwa kikao cha kazi na mwenzake mwenye dhamana ya Hidrokaboni Didier Budimbu, Jumatano Januari 19.

Maeneo ya mashariki na kusini mwa nchi yanakabiliwa na uhaba mafuta na kupanda kwa bei ya mafuta. Uhaba huu unaathiri usafiri wa umma na shughuli nyingine za kiuchumi zinazotegemea mafuta.
Maeneo ya mashariki na kusini mwa nchi yanakabiliwa na uhaba mafuta na kupanda kwa bei ya mafuta. Uhaba huu unaathiri usafiri wa umma na shughuli nyingine za kiuchumi zinazotegemea mafuta. © RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

“Tunaomba wamiliki wa kampuni za mafuta wawe watulivu, kwa sababu serikali imejipanga kuleta utulivu katika sekta yao na katika kipindi cha saa 48 tutakuwa na muundo mpya wa bei na kila mmoja atazindua upya shughuli zake”, ametangaza Jean-Marie Kalumba kulingana na Rdaio OKAPI.

Amebainisha kuwa tatizo la hisa na ukosefu wa faida ndilo kiini cha uhaba huo. Hata hivyo, serikali imefanya mazungumzo na wadau wa uchumi katika sekta hiyo.

“Haya ni masuala ambayo tutayatatua. Katika kipindi cha saa 48 tutapata suluhisho. Jana tulikuwa na mkutano na wadau wa uchumi katika sekta ya mafuta. Tuko katika mchakato wa kurekebisha miundo ya bei. Tatizo tulilonalo ni la hisa. Katika mkoa wa Katanga, hakuna mafuta na hilo halina hoja. Tunalifanyia kazi hilo. Hadi wakati huo, tutalipa hasara na mapungufu, "aliahidi Jean-Marie Kalumba.

Maeneo ya mashariki na kusini mwa nchi yanakabiliwa na uhaba mafuta na kupanda kwa bei ya mafuta. Uhaba huu unaathiri usafiri wa umma na shughuli nyingine za kiuchumi zinazotegemea mafuta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.