Pata taarifa kuu
NIGER-DIPLOMASIA

Niger: Hatua ya kufukuzwa kwa Wanyarwanda 8, yasitishwa

Wanyarwanda hawa waliokuwa vigogo wa utawala wa Kihutu, wanane walihukumiwa au kuachiliwa huru na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ya Rwanda (ICTR) kwa jukumu lao katika mauaji ya kimbari. Walikuwa wakiishi Tanzania na Niger ilikubali kuwachukua mwezi Novemba mwaka jana, chini ya makubaliano na Umoja wa Mataifa kabla ya kurejelea uamuzi wao.

Ofisi za Mahakama ya Kimataifa ya Rwanda mjini Arusha.
Ofisi za Mahakama ya Kimataifa ya Rwanda mjini Arusha. (CC)/Tomsudani/Wikipédia
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa uliiamuru Niamey kusitisha uamuzi wake wa kuwafukuza raia hao wanane wa Rwanda.

Wanyarwanda hawa waliwasili Niger mnamo Desemba 6 kama sehemu ya makubaliano ya kuhamisha yaliyotiwa saini na mamlaka ya Niger na Umoja wa Mataifa mwezi mmoja mapema.

Lakini sasa, mara tu walipofika, Wanyarwanda hawa wanane walitangaziwa kufukuzwa kwao ndani ya siku saba, kwenda kusikojulikana, kwa sababu za "kidiplomasia".

Taasisi ya Umoja wa Mataifa, inaoshughulikia uhamisho wa watu waliofikishwa mbele ya ICTR, ilijibu mara moja.

Katika barua taasisi hiyo iliomba Niger kuruhusu watu hawa kusalia katika ardhi yake "kulingana na masharti ya makubaliano", na hadi "uamuzi wa mwisho juu ya suala hili".

Kulingana na chombo cha habari cha Jeune Afrique, Niamey ilirejelea uamuzi wake wa kuwapokea Wanyarwanda hao kutokana na Rwanda kuonyesha kutoridhika kwake na uamuzi huo.

Miongoni mwa viongozi wanane wa zamani, wanne waliachiwa huru na ICTR - akiwemo kaka yake Agathe Habyarimana, mke wa rais wa zamani wa Rwanda. Wengine wanne wametumikia kifungo ambacho ICTR iliwahukumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.