Pata taarifa kuu

Nyota wa mitindo ya Rumba ya DRC Jenerali Défao afariki dunia

Jenerali Défao alifariki Jumatatu nchini Cameroon baada ya afya yake kuzorota. Angelitimiza umri wa miaka 63 Desemba 31. Mwanamuziki huyu mahiri aliwasili nchini Cameroon wiki jana kutumbwiza kwenye tamasha kubwa la muziki.

Mwanamuziki nguli wa mitindo ya Rumba Jenerali Défao.
Mwanamuziki nguli wa mitindo ya Rumba Jenerali Défao. © Capture d'écran Youtube
Matangazo ya kibiashara

Jenerali Défao ambaye jina lake halisi ni Lulendo Matumona, alifariki katika hospitali huko Douala. Kulingana na gazeti la kila siku la Kinshasa La Référence Plus, msanii huyo alikuwa mwathirika wa matatizo ya kiafya: kisukari kilichochanganyika na Covid-19. Mara tu alipofika Cameroon, aliummwa na kuzirai na mara moja alipelekwa hadi kituo cha matibabu cha Laquintinie.

Ni mwanamuziki mahiri aliyeifanya Afrika nzima kucheza densi, amesema Tom Mpiana, mshirika wake wa karibu.

Tom Mpiana anakumbusha nyimbo ambazo zilipata sifa na kumfanya Jenerali Défao kuwa maarufua kama vile Radio trottoir, Famille Kikuta au Amour scolaire.

Jenerali Défao alianza muziki mwaka wa 1976 huko Matadi katika bendi za mitaani. Kati ya mwaka wa 1983 na 1991, alifanikiwa kujiunga na bendi za Zaïko Wawa na Choc Stars kabla ya kuanzisha bendi yake mwenyewe ya Big Stars, mwaka 1991.

Jenerali Défao pia aliimba pamoja na watu wengine mashuhuri kama vile Carlito na Debaba. Na wapenzi wengi wa muziki watakumbuka kwa muda mrefu muziki aliyocheza na mwanamuziki maarufu Mbilia Belle katika kumuuenzi hayati Simaro Lutumba Ndomanueno.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.