Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

DRC: Rais Tshisekedi asakata uthabiti wa kisiasa mikoani

Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi amewataka magavana kwenye majimbo ya nchi hiyo kushirikiana na mabunge yao katika kukuza mshikamano wa kitaifa na umoja.

Rais wa DRC Félix Tshisekedi.
Rais wa DRC Félix Tshisekedi. Sumy Sadurni / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tshisekedi ametoa rai hiyo kwa magavana wa majimbo kufanya kazi kwa ushirikiano na mabunge yao wakati wa ufunguzi wa kikao cha 8 cha kongamano la magavana linaloendelea jijini Kinshasa huku akiwataka magavana wa mikowa yote 26 kutafuta suluhu ya migogoro ya kisiasa inayoshuhudiwa katika maeneo kadhaa nchini Humo.

Pamoja na kukiri kudorora kwa uchumi, lakini pia kukosekana kwa mipango mikakati ya kuboresha maisha ya raia kwenye majimbo, hali inayosababisha wabunge kwenye majimbo kutokuwa na imani kwa magavana hadi kuwafuta kazi, rais Tshisekedi amesema ni hali inayoeleweka lakini lazima kuwe na ushirikishwaji wa kila sekta, kwa ajili ya maendeleo ya jamii.

Kongamano hili limeandaliwa na idara ya kitaifa inayojihusisha na utawala wa majimbo katika wizara ya mambo ya ndani, chini ya kauli mbiu inayosema Utulivu katika tawala za majimbo, hakikisho la mafanikio ya mpango wa maendeleo ya jamii lililoanzishwa hapo siku ya jumatano wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.