Pata taarifa kuu
MALI-USHIRIKIANO

Mali: Assimi Goïta kukutana na Emmanuel Macron Desemba 20

Rais wa Ufaransa atakutana na Kanali Assimi Goïta, rais wa mpito wa Mali. Hii ni mara ya kwanza kwa marais hao wawili kuzungumza ana kwa ana baada ya mazungumzo kadhaa ya simu.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa mpito wa Mali Assimi Goïta.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa mpito wa Mali Assimi Goïta. © AP - Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo umepangwa kufanyika Jumatatu, Desemba 20 huko Bamako, kulingana na taarifa kutoka Gazeti la Jeune Afrique, taarifa ambayo RFI iliweza kuthibitisha kutoka Ikulu ya Elysée. Mazunguzo ya viongozi hao yatagubikwa na masuala mengi.

Ni katika hali ya wasiwasi wa kidiplomasia ambapo Assimi Goïta atampokea Emmanuel Macron huko Bamako, mji mkuu wa Mali, katika siku  chache zijazo. Rais wa Ufaransa anatarajiwa kufanya ziara hiyo nchini Mali Jumatatu, Desemba 20. Ziara hii inakuja wakati vikosi vya Ufaransa vya Barkhane vinarejea nyumbani kutoka Mali, wakati kuna uwezekano wa kuwasili kwa wanamgambo wa Kirusi nchini humo au hata muda wa mpito wa Mali ukiendelea kuzua wasiwasia.

Kwa miezi kadhaa nchi hizi mbili zimekuwa zikitupiana maneneo. Mali, kupitia Waziri wake Mkuu wa kipindi cha mpito Choguel Maïga, ilitaja kumalizika kwa Operesheni Barkhane kama "kutelekezwa kabisa" kwa nchi hiyo mbele ya Umoja wa Mataifa. Maneno yaliyotajwa na Emmanuel Macron kama "aibu" .  Wakati huo Rais Mcaron alitilia shaka uaminifu wa serikali ya Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.