Pata taarifa kuu

Ethiopia: Human Rights Watch yahusisha waasi wa Tigray kwa mauaji ya raia

Kulingana na shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, vikosi vya Tigray viliwaua kikatili makumi ya raia mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.

Wapiganaji wa vikosi vya waasi wa Tigray nchini Ethiopia, Juni 2021.
Wapiganaji wa vikosi vya waasi wa Tigray nchini Ethiopia, Juni 2021. AFP - YASUYOSHI CHIBA
Matangazo ya kibiashara

Kwa jumla, karibu watu 50 waliuawa muda mfupi baada ya kuwasili kwa vikosi vya Tigray katika miji ya Chenna na Kobo kaskazini mwa mkoa wa Ahmara. Mauaji ambayo yanaonekana kuwa ni uhalifu wa kivita.

"Vikosi vya Tigrayan viliingia katika nyumba za watu binafsi, vilitumia maeneo haya kupigana na majeshi ya Ethiopia na kuamua kuua mtu mmoja au wawili wa familia," amesema Gerry Simpson, naibu mkurugenzi wa kitengo cha migogoro na mizozo katika shirika la Human Rights Watch. KItendo hiki kilitokea kwa sababu raia walikataa kuwalisha, au kwa sababu walishuku kwamba mmoja wao alikuwa na uhusiano fulani na mtu mwingine ambaye alikuwa sehemu ya wanajeshi wa Ethiopia au wanamgambo wanaopigana kwa upande wa majeshi ya Ethiopia. "

Uporaji mkubwa wa Hifadhi ya chakula

"Tunatoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuanzisha uchunguzi huru wa kimataifa," anaendelea Gerry Simpson, "kuchunguza na kulaani ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na pande zote katika vita hivi, sio tu vikosi vya Tigray bali pia vikosi vya Ethiopia na Eritrea. "

Hata hivyo, waasi wa Tigray walikanusha, Ijumaa, Desemba 10, kuhusika na visa vyovyote vya uporaji wa Hifadhi ya chakula huko Kombolcha. Siku ya Alhamisi, msemaji wa Umoja wa Mataifa alitangaza kuwa usambazaji wa chakula cha msaada utasitishwa baada ya uporaji mkubwa wa chakula katika mji wa mkoa wa Ahmara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.