Pata taarifa kuu
DRC-UCHUMI

IMF yaipongeza DRC kwa hatua ambayo imefikia kuhusu mageuzi muhimu ya kiuchumi

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha duniani IMF, Kristalina Georgieva, anamaliza ziara yake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya kukutana na rais Felix Tshisekedi, na kujadiliana kuhusu hali ya kiuchumi nchini humo.

Bi. Georgieva amesema DRC inaimarika kiuchumi kufuatia mageuzi muhimu ya kiuchumi, yanayotekelezwa na serikali ya Tshisekedi ikiwa ni pamoja na mikakati mipya ya ukusanyaji wa kodi na kudhibiti matumizi ya fedha za umma.
Bi. Georgieva amesema DRC inaimarika kiuchumi kufuatia mageuzi muhimu ya kiuchumi, yanayotekelezwa na serikali ya Tshisekedi ikiwa ni pamoja na mikakati mipya ya ukusanyaji wa kodi na kudhibiti matumizi ya fedha za umma. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Mkuu huyo wa IMF amesifia mipango ya kiuchumi iliyowekwa na rais Tshisekedi wakati huu uchumi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ukitarajiwa kukua kwa asilimia 6.4 ifikapo mwaka 2022.

Bi. Georgieva amesema DRC inaimarika kiuchumi kufuatia mageuzi muhimu ya kiuchumi, yanayotekelezwa na serikali ya Tshisekedi ikiwa ni pamoja na mikakati mipya ya ukusanyaji wa kodi na kudhibiti matumizi ya fedha za umma.

Wakati dunia inapoadhimisha siku ya kimataifa ya kupambana na ufisadi, suala hilo pia lilijadiliwa kati ya viongozi hao, huku Bi. Georgieva akimpongeza rais Tshisekedi kwa jitihada zake za kuimarisha uongozi bora hasa kuimarisha sekta ya madini humo kwa kuifanyia mageuzi.

Mwezi Julai, IMF ilitangaza kuipa DRC mkopo wa Dola Bilioni 1.5 kwa kipindi cha miaka mitatu, kwa sharti la kuifanyia mageuzi sekta ya madini nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.